Methali 15:1-7
Methali 15:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Kujibu kwa upole hutuliza hasira, lakini neno kali huchochea hasira. Ulimi wa mwenye hekima hueneza maarifa, lakini watu wapumbavu hububujika upuuzi. Macho ya Mwenyezi-Mungu huona kila kitu, humchunguza mtu mwema na mtu mbaya. Ulimi mpole ni chanzo cha uhai, lakini uovu wake huvunja moyo. Mpumbavu hudharau mafundisho ya baba yake, lakini anayekubali maonyo ana busara. Nyumbani mwa mwadilifu mna wingi wa mali, lakini mapato ya waovu huishia na balaa. Mdomo wa mwenye hekima hueneza maarifa, lakini sivyo ilivyo mioyo ya wapumbavu.
Methali 15:1-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu. Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu. Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema. Ulimi safi ni mti wa uzima; Bali ukorofi wa ulimi huvunja moyo. Mpumbavu hudharau kurudiwa na babaye; Bali yeye aangaliaye maonyo hupata busara. Katika nyumba ya mwenye haki mna akiba nyingi; Bali mapato ya mtu mbaya huwa taabu tu. Midomo ya mwenye haki hueneza maarifa; Bali moyo wa mpumbavu haufanyi hivyo.
Methali 15:1-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu. Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu. Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema. Ulimi safi ni mti wa uzima; Bali ukorofi wa ulimi huvunja moyo. Mpumbavu hudharau kurudiwa na babaye; Bali yeye aangaliaye maonyo hupata busara. Katika nyumba ya mwenye haki mna akiba nyingi; Bali mapato ya mtu mbaya huwa taabu tu. Midomo ya mwenye haki hueneza maarifa; Bali moyo wa mpumbavu haufanyi hivyo.
Methali 15:1-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Jawabu la upole hugeuza ghadhabu, bali neno liumizalo huchochea hasira. Ulimi wa mwenye hekima husifu maarifa, bali kinywa cha mpumbavu hufoka upumbavu. Macho ya BWANA yako kila mahali, yakiwaangalia waovu na wema. Ulimi uletao uponyaji ni mti wa uzima, bali ulimi udanganyao huponda roho. Mpumbavu hubeza maonyo ya baba yake, bali yeyote akubaliye maonyo huonesha busara. Nyumba ya mwenye haki ina hazina kubwa, bali mapato ya waovu huwaletea taabu. Midomo ya mwenye hekima hueneza maarifa, bali sivyo ilivyo mioyo ya wapumbavu.