Methali 14:3-4
Methali 14:3-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Mpumbavu hujiadhibu mwenyewe kwa kuropoka kwake, lakini mwenye hekima hulindwa na maneno yake. Bila ng'ombe wa kulima ghala za mtu ni tupu, mavuno mengi hupatikana kwa nguvu ya ng'ombe wa kulima.
Shirikisha
Soma Methali 14Methali 14:3-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Katika kinywa cha mpumbavu mna fimbo ya kiburi, Bali midomo ya wenye hekima huwahifadhi. Zizi ni safi ambapo hapana ng'ombe; Bali nguvu za ng'ombe zaleta faida nyingi.
Shirikisha
Soma Methali 14