Methali 14:1-4
Methali 14:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, lakini mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe. Mwenye mwenendo mnyofu humcha Mwenyezi-Mungu, lakini mpotovu humdharau Mungu. Mpumbavu hujiadhibu mwenyewe kwa kuropoka kwake, lakini mwenye hekima hulindwa na maneno yake. Bila ng'ombe wa kulima ghala za mtu ni tupu, mavuno mengi hupatikana kwa nguvu ya ng'ombe wa kulima.
Methali 14:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe. Yeye aendaye kwa unyofu wake humcha BWANA; Bali aliye mkaidi katika njia zake humdharau. Katika kinywa cha mpumbavu mna fimbo ya kiburi, Bali midomo ya wenye hekima huwahifadhi. Zizi ni safi ambapo hapana ng'ombe; Bali nguvu za ng'ombe zaleta faida nyingi.
Methali 14:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe. Yeye aendaye kwa unyofu wake humcha BWANA; Bali aliye mkaidi katika njia zake humdharau. Katika kinywa cha mpumbavu mna fimbo ya kiburi, Bali midomo ya wenye hekima huwahifadhi. Zizi ni safi ambapo hapana ng’ombe; Bali nguvu za ng’ombe zaleta faida nyingi.
Methali 14:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, bali mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe. Yeye ambaye njia zake ni nyofu humcha BWANA, bali yeye ambaye njia zake zimepotoka humdharau Mungu. Mazungumzo ya mpumbavu huleta fimbo mgongoni mwake, bali mwenye hekima hulindwa na maneno ya midomo yake. Pale ambapo hakuna mafahali, hori ni tupu, bali kutokana na nguvu za fahali huja mavuno mengi.