Methali 13:20-25
Methali 13:20-25 Biblia Habari Njema (BHN)
Anayeandamana na wenye hekima hupata hekima, lakini anayejiunga na wapumbavu atapata madhara. Watendao dhambi huandamwa na balaa, lakini waadilifu watatuzwa mema. Mtu mwema huwaachia urithi uzao wake, lakini mali ya mwenye dhambi imerundikiwa waadilifu. Shamba la maskini hutoa mazao mengi, lakini bila haki hunyakuliwa. Asiyemwadhibu mtoto wake hampendi; lakini ampendaye mwanawe humrudi mapema. Mwadilifu anacho chakula cha kumtosheleza, lakini tumbo la waovu hutaabika kwa njaa.
Methali 13:20-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia. Uovu huwafuatia wenye dhambi; Bali mwenye haki atalipwa mema. Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki. Chakula kingi chapatikana kwa ukulima wa maskini; Bali viko viharibiwavyo kwa sababu ya dhuluma. Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema. Mwenye haki hula akaishibisha nafsi yake; Bali tumbo la mtu mbaya litaona njaa.
Methali 13:20-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia. Uovu huwaandamia wenye dhambi; Bali mwenye haki atalipwa mema. Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki. Chakula kingi chapatikana kwa ukulima wa maskini; Bali viko viharibiwavyo kwa sababu ya dhuluma. Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema. Mwenye haki hula akaishibisha nafsi yake; Bali tumbo la mtu mbaya litaona njaa.
Methali 13:20-25 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Yeye atembeaye na mwenye hekima atapata hekima, bali rafiki wa mpumbavu hupata madhara. Balaa humwandama mtenda dhambi, bali mafanikio ni thawabu kwa mwenye haki. Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi, bali mali ya wenye dhambi imehifadhiwa kwa ajili ya wenye haki. Shamba la mtu maskini laweza kuzalisha chakula kingi, bali dhuluma hukifutilia mbali. Yeye asiyetumia fimbo yake hampendi mwanawe, bali yeye ampendaye huwa mwangalifu kumwadibisha. Mwenye haki hula hadi akaridhisha moyo wake, bali tumbo la mwovu hutaabika kwa njaa.