Methali 13:17-19
Methali 13:17-19 Biblia Habari Njema (BHN)
Mjumbe mbaya huwatumbukiza watu taabuni, lakini mjumbe mwaminifu huleta nafuu. Umaskini na fedheha humpata asiyejali mafundisho, lakini mwenye kusikia maonyo huheshimiwa. Inafurahisha upatapo kile unachotaka, kwa hiyo wapumbavu huchukia kuepa uovu.
Methali 13:17-19 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mjumbe mbaya huanguka maovuni; Bali mjumbe mwaminifu ni afya. Umaskini na fedheha zitampata yeye akataaye kurudiwa; Bali yeye aangaliaye maonyo ataheshimiwa. Haja iliyopatikana ni tamu nafsini mwa mtu; Bali kujitenga na maovu ni chukizo kwa wapumbavu.
Methali 13:17-19 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mjumbe mbaya huanguka maovuni; Bali mjumbe mwaminifu ni afya. Umaskini na fedheha zitampata yeye akataaye kurudiwa; Bali yeye aangaliaye maonyo ataheshimiwa. Haja iliyopatikana ni tamu nafsini mwa mtu; Bali kujitenga na maovu ni chukizo kwa wapumbavu.
Methali 13:17-19 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mjumbe mwovu huanguka kwenye taabu, bali mjumbe mwaminifu huleta uponyaji. Yeye anayedharau maonyo hupata umaskini na aibu, bali yeye anayekubali maonyo huheshimiwa. Tarajio lililotimizwa ni tamu kwa nafsi, bali wapumbavu huchukia sana kuacha ubaya.