Methali 13:12-14
Methali 13:12-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Tumaini la kungojangoja huumiza moyo, lakini tazamio linalotimia ni mti wa uhai. Anayedharau mawaidha anajiletea maangamizi, lakini anayetii amri atapewa tuzo. Mafundisho ya wenye hekima ni chemchemi ya uhai; humwezesha mtu kuiepa mitego ya kifo.
Methali 13:12-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua. Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima. Kila anayelidharau neno hujiletea uharibifu; Bali yeye anayeiogopa amri atapewa thawabu. Sheria ya mwenye akili ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti.
Methali 13:12-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua. Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima. Kila alidharauye neno hujiletea uharibifu; Bali yeye aiogopaye amri atapewa thawabu. Sheria ya mwenye akili ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti.
Methali 13:12-14 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua, bali tumaini lililotimizwa ni mti wa uzima. Yeye anayedharau mafundisho anajiletea maangamizi, bali yeye anayeheshimu agizo hupewa tuzo. Mafundisho ya mwenye busara ni chemchemi ya uzima, ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti.