Methali 12:21-23
Methali 12:21-23 Biblia Habari Njema (BHN)
Waadilifu hawapatwi na jambo lolote baya, lakini waovu wamejaa dhiki. Midomo isemayo uongo ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, lakini watu waaminifu ni furaha yake. Mwenye busara huficha maarifa yake, lakini wapumbavu hutangaza upumbavu wao.
Methali 12:21-23 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwenye haki hatapatikana na msiba wowote; Bali wasio haki watajazwa mabaya. Midomo ya uongo ni chukizo kwa BWANA; Bali watendao uaminifu ndio furaha yake. Mwanadamu mwenye busara husitiri maarifa; Bali moyo wa wapumbavu hutangaza upumbavu.
Methali 12:21-23 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwenye haki hatapatikana na msiba wo wote; Bali wasio haki watajazwa mabaya. Midomo ya uongo ni chukizo kwa BWANA; Bali watendao uaminifu ndio furaha yake. Mwanadamu mwenye busara husitiri maarifa; Bali moyo wa wapumbavu hutangaza upumbavu.
Methali 12:21-23 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hakuna dhara linalompata mwenye haki, bali waovu wana taabu nyingi. BWANA anachukia sana midomo idanganyayo, bali hufurahia watu ambao ni wa kweli. Mtu mwenye busara hujihifadhia maarifa yeye mwenyewe, bali moyo wa wapumbavu hububujika upumbavu.