Methali 11:23-25
Methali 11:23-25 Biblia Habari Njema (BHN)
Matazamio ya waadilifu yana matokeo mema; tamaa za waovu huishia katika ghadhabu. Atoaye kwa ukarimu huzidi kutajirika; lakini bahili huzidi kudidimia katika umaskini. Mtu mkarimu atafanikishwa, amnyweshaye mwingine maji naye atanyweshwa.
Methali 11:23-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Haja ya mwenye haki ni kupata mema tu; Bali kutaraji kwake mtu mwovu huishia katika ghadhabu. Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji. Nafsi ya mtu mkarimu itastawishwa; Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe.
Methali 11:23-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Haja ya mwenye haki ni mema tu; Bali kutaraji kwake mtu mwovu ni ghadhabu. Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji. Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa; Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe.
Methali 11:23-25 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Shauku ya mwenye haki huishia tu kwenye mema, bali tumaini la mwovu huishia tu kwenye ghadhabu. Kuna mtu atoaye kwa ukarimu, hata hivyo hupata zaidi, mwingine huzuia, lakini huwa maskini. Mtu mkarimu atastawi; yeye awaburudishaye wengine ataburudishwa mwenyewe.