Methali 11:1-6
Methali 11:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Mizani ya udanganyifu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, lakini matumizi ya kipimo halali ni furaha kwake. Kiburi huandamana na fedheha, lakini kwa watu wanyenyekevu mna hekima. Unyofu wa watu wema huwaongoza, upotovu wa wenye hila huwaangamiza. Utajiri haufai kitu siku ya ghadhabu, lakini uadilifu huokoa kutoka kifo. Uadilifu wa watu wanyofu huinyosha njia yao, lakini waovu huanguka kwa uovu wao wenyewe. Uadilifu wa wanyofu huwaokoa na hatari, lakini wafitini hunaswa kwa tamaa zao wenyewe.
Methali 11:1-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mizani ya udanganyifu ni chukizo kwa BWANA; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza. Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu. Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza. Mali hazifaidii kitu siku ya ghadhabu; Bali haki huokoa na mauti. Haki yake mtu mkamilifu itamwongoza njia yake; Bali mtu mwovu ataanguka kwa uovu wake. Haki yao wenye haki itawaokoa; Bali wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe.
Methali 11:1-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mizani ya hadaa ni chukizo kwa BWANA; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza. Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu. Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza. Mali hazifaidii kitu siku ya ghadhabu; Bali haki huokoa na mauti. Haki yake mtu mkamilifu itamwongoza njia yake; Bali mtu mwovu ataanguka kwa uovu wake. Haki yao wenye haki itawaokoa; Bali wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe.
Methali 11:1-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
BWANA huchukia sana mizani za udanganyifu, bali vipimo sahihi ni furaha yake. Kiburi kinapokuja, ndipo huja aibu, bali unyenyekevu huja na hekima. Uadilifu wa wenye haki huwaongoza, bali wasio waaminifu huangamizwa na hila yao. Utajiri haufaidi kitu katika siku ya ghadhabu, bali haki huokoa kutoka mautini. Haki ya wasio na lawama, huwatengenezea njia iliyo nyofu, bali waovu huangushwa kwa uovu wao wenyewe. Haki ya wanyofu huwaokoa, bali wasio waaminifu hunaswa na tamaa mbaya.