Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 11:1-31

Methali 11:1-31 Biblia Habari Njema (BHN)

Mizani ya udanganyifu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, lakini matumizi ya kipimo halali ni furaha kwake. Kiburi huandamana na fedheha, lakini kwa watu wanyenyekevu mna hekima. Unyofu wa watu wema huwaongoza, upotovu wa wenye hila huwaangamiza. Utajiri haufai kitu siku ya ghadhabu, lakini uadilifu huokoa kutoka kifo. Uadilifu wa watu wanyofu huinyosha njia yao, lakini waovu huanguka kwa uovu wao wenyewe. Uadilifu wa wanyofu huwaokoa na hatari, lakini wafitini hunaswa kwa tamaa zao wenyewe. Mwovu akifa tumaini lake nalo hutoweka; tazamio la asiyemcha Mungu huishia patupu. Mtu mnyofu huokolewa katika shida, na mwovu huingia humo badala yake. Asiyemcha Mungu huangamiza wengine kwa mdomo wake, lakini mwadilifu huokolewa kwa maarifa yake. Waadilifu wakipata fanaka mji hushangilia, na waovu wakiangamia watu hupiga vigelegele. Mji hufanikishwa kwa baraka za wanyofu, lakini huangamizwa kwa mdomo wa waovu. Anayemdharau jirani yake hana akili, mtu mwenye busara hukaa kimya. Apitapitaye akichongea hutoa siri, lakini anayeaminika rohoni huficha siri. Pasipo na uongozi taifa huanguka, penye washauri wengi pana usalama. Anayemdhamini mgeni atakuja juta, lakini anayechukia mambo ya dhamana yu salama. Mwanamke mwema huheshimiwa, mwanamume mwenye bidii hutajirika. Mtu mkarimu hufaidika yeye mwenyewe, lakini mtu mkatili hujiumiza mwenyewe. Faida anayopata mwovu ni ya uongo, lakini atendaye mema hakika atapata faida ya kweli. Mtu anayepania kuwa mwadilifu ataishi, lakini anayechagua kutenda maovu atakufa. Wenye nia mbaya ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, lakini wenye mwenendo mwema ni furaha yake. Hakika mwovu hataepa kuadhibiwa, lakini waadilifu wataokolewa. Mwanamke mzuri asiye na akili, ni kama pete ya dhahabu puani mwa nguruwe. Matazamio ya waadilifu yana matokeo mema; tamaa za waovu huishia katika ghadhabu. Atoaye kwa ukarimu huzidi kutajirika; lakini bahili huzidi kudidimia katika umaskini. Mtu mkarimu atafanikishwa, amnyweshaye mwingine maji naye atanyweshwa. Watu humlaani afichaye nafaka, lakini humtakia baraka mwenye kuiuza. Atafutaye kutenda mema hupata fadhili, lakini atafutaye kutenda maovu atapatwa na maovu. Anayetegemea mali zake ataanguka, lakini mwadilifu atastawi kama jani bichi. Anayeivunja nyumba yake ataambua upepo. Mpumbavu atakuwa mtumwa wa wenye hekima. Matendo ya mwadilifu huleta uhai, lakini uhalifu huuondoa uhai. Ikiwa mwadilifu hupata tuzo hapa duniani, hakika mwovu na mwenye dhambi atapatilizwa.

Shirikisha
Soma Methali 11

Methali 11:1-31 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Mizani ya udanganyifu ni chukizo kwa BWANA; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza. Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu. Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza. Mali hazifaidii kitu siku ya ghadhabu; Bali haki huokoa na mauti. Haki yake mtu mkamilifu itamwongoza njia yake; Bali mtu mwovu ataanguka kwa uovu wake. Haki yao wenye haki itawaokoa; Bali wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe. Mtu mwovu atakapokufa, taraja lake linapotea; Na matumaini ya uovu huangamia. Mwenye haki huokolewa katika dhiki, Na mtu mwovu ataiingia badala yake. Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa kinywa chake; Bali wenye haki watapona kwa maarifa. Wenye haki wasitawipo, mji hufurahi; Waovu wanapoangamia, watu hushangilia. Mji hutukuzwa kwa mbaraka wa mwenye haki; Bali mji hupinduliwa kwa kinywa cha mwovu. Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza. Mwenye udaku hupitapita akifunua siri; Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo. Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu. Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia; Achukiaye mambo ya dhamana yuko salama. Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; Na watu wakali hushika mali siku zote. Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake; Aliye mkali hujisumbua mwili wake. Mtu mwovu hupata mshahara wa udanganyifu; Apandaye haki ana thawabu ya hakika. Haki huelekea uzima; Afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe. Wenye uhalifu moyoni ni chukizo kwa BWANA; Walio wakamilifu katika njia zao humpendeza. Hakika, mtu mwovu hatakosa adhabu; Bali wazawa wa wenye haki wataokoka. Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, Ndivyo alivyo mwanamke mzuri asiye na akili. Haja ya mwenye haki ni kupata mema tu; Bali kutaraji kwake mtu mwovu huishia katika ghadhabu. Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji. Nafsi ya mtu mkarimu itastawishwa; Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe. Awanyimaye watu nafaka, watu watamlaani; Auzaye nafaka, baraka itakuwa kichwani pake. Atafutaye mema kwa bidii hutafuta fadhili; Atafutaye madhara, hayo yatamjia. Azitegemeaye mali zake ataanguka; Mwenye haki atasitawi kama jani. Ataabishaye nyumba yake mwenyewe ataurithi upepo; Mpumbavu atakuwa mtumwa wa mtu mwenye moyo wa akili. Mazao ya mwenye haki ni mti wa uzima; Na mwenye hekima huvuta roho za watu. Ikiwa, mwenye haki atalipwa duniani; Je, mwovu na mkosaji hawatalipwa mara nyingi zaidi?

Shirikisha
Soma Methali 11

Methali 11:1-31 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Mizani ya hadaa ni chukizo kwa BWANA; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza. Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu. Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza. Mali hazifaidii kitu siku ya ghadhabu; Bali haki huokoa na mauti. Haki yake mtu mkamilifu itamwongoza njia yake; Bali mtu mwovu ataanguka kwa uovu wake. Haki yao wenye haki itawaokoa; Bali wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe. Mtu mwovu atakapokufa, taraja lake lapotea; Na matumaini ya uovu huangamia. Mwenye haki huokolewa katika dhiki, Na mtu mwovu ataiingia badala yake. Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa kinywa chake; Bali wenye haki watapona kwa maarifa. Wenye haki wasitawipo, mji hufurahi; Waovu waangamiapo, watu hupiga kelele. Mji hutukuzwa kwa mbaraka wa mwenye haki; Bali mji hupinduliwa kwa kinywa cha mwovu. Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza. Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo. Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu. Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia; Achukiaye mambo ya dhamana yu salama. Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; Na watu wakali hushika mali siku zote. Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake; Aliye mkali hujisumbua mwili wake. Mtu mwovu hupata mshahara wa udanganyifu; Apandaye haki ana thawabu ya hakika. Haki huelekea uzima; Afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe. Wenye kuhalifu moyoni ni chukizo kwa BWANA; Walio wakamilifu katika njia zao humpendeza. Hakika, mtu mwovu hatakosa adhabu; Bali wazao wa wenye haki wataokoka. Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, Kadhalika mwanamke mzuri asiye na akili. Haja ya mwenye haki ni mema tu; Bali kutaraji kwake mtu mwovu ni ghadhabu. Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji. Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa; Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe. Awanyimaye watu nafaka, watu watamlaani; Auzaye nafaka, baraka itakuwa kichwani pake. Atafutaye mema kwa bidii hutafuta fadhili; Atafutaye madhara, hayo yatamjia. Azitegemeaye mali zake ataanguka; Mwenye haki atasitawi kama jani. Ataabishaye nyumba yake mwenyewe ataurithi upepo; Mpumbavu atakuwa mtumwa wa mtu mwenye moyo wa akili. Mazao ya mwenye haki ni mti wa uzima; Na mwenye hekima huvuta roho za watu. Tazama, mwenye haki atalipwa duniani; Basi mwovu na mkosaji si mara nyingi zaidi?

Shirikisha
Soma Methali 11

Methali 11:1-31 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

BWANA huchukia sana mizani za udanganyifu, bali vipimo sahihi ni furaha yake. Kiburi kinapokuja, ndipo huja aibu, bali unyenyekevu huja na hekima. Uadilifu wa wenye haki huwaongoza, bali wasio waaminifu huangamizwa na hila yao. Utajiri haufaidi kitu katika siku ya ghadhabu, bali haki huokoa kutoka mautini. Haki ya wasio na lawama, huwatengenezea njia iliyo nyofu, bali waovu huangushwa kwa uovu wao wenyewe. Haki ya wanyofu huwaokoa, bali wasio waaminifu hunaswa na tamaa mbaya. Matumaini yaliyo katika wanadamu hufa pamoja nao; ahadi zote za uwezo wao hubatilika. Mtu mwenye haki huokolewa kutoka taabu, naye mtu mwovu huingia humo badala yake. Kwa kinywa chake mtu asiyemwamini Mungu humwangamiza jirani yake, bali kwa maarifa mwenye haki huokolewa. Mwenye haki anapofanikiwa, mji hufurahi; mwovu anapoangamia, kuna shangwe za furaha. Kutokana na baraka ya mtu mnyofu mji hukwezwa, bali kwa kinywa cha mwovu mji huharibiwa. Mtu asiye na akili humdharau jirani yake, bali mtu mwenye ufahamu huuzuia ulimi wake. Masengenyo husaliti uaminifu, bali mtu mwaminifu hutunza siri. Pasipo ushauri wa hekima taifa huanguka, bali washauri wengi hufanya ushindi uwe wa hakika. Yeye amdhaminiye mgeni hakika atateseka, bali yeyote akataaye kuunga mkono dhamana ni salama. Mwanamke mwenye moyo wa huruma hupata heshima, bali wanaume wakorofi hupata mali tu. Mwenye huruma hujinufaisha mwenyewe, bali mkatili hujiletea taabu mwenyewe. Mtu mwovu hupata ujira wa udanganyifu, bali yeye apandaye haki huvuna tuzo ya uhakika. Mtu mwenye haki kweli kweli hupata uzima, bali yeye afuatiliaye ubaya huendea kifo chake. BWANA huwachukia sana watu wenye moyo wa upotovu, bali hupendezwa na wale ambao njia zao hazina lawama. Uwe na hakika na hili: Waovu hawataepuka kuadhibiwa, bali wenye haki watakuwa huru. Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe ndivyo alivyo mwanamke mzuri ambaye hana busara. Shauku ya mwenye haki huishia tu kwenye mema, bali tumaini la mwovu huishia tu kwenye ghadhabu. Kuna mtu atoaye kwa ukarimu, hata hivyo hupata zaidi, mwingine huzuia, lakini huwa maskini. Mtu mkarimu atastawi; yeye awaburudishaye wengine ataburudishwa mwenyewe. Watu humlaani mtu awanyimae watu nafaka, bali baraka itamkalia kichwani kama taji yeye aliye radhi kuiuza. Yeye atafutaye mema hupata ukarimu, bali ubaya huja kwake yeye autafutaye. Yeyote ategemeaye utajiri wake ataanguka, bali mwenye haki atastawi kama jani bichi. Yeye aletaye taabu kwa jamaa yake atarithi tu upepo, naye mpumbavu atakuwa mtumishi wa wenye hekima. Tunda la mwenye haki ni mti wa uzima, naye mwenye hekima huokoa maisha. Kama wenye haki watapokea ujira wao duniani, si zaidi sana mtu asiyemcha Mungu, na mwenye dhambi?

Shirikisha
Soma Methali 11