Methali 10:2-5
Methali 10:2-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Mali iliyopatikana kwa njia mbaya haifai, lakini uadilifu huokoa mtu kutoka kifoni. Mwenyezi-Mungu hawaachi waadilifu wapate njaa, lakini huzipinga tamaa za waovu. Uvivu husababisha umaskini, lakini mkono wa mtu wa bidii hutajirisha. Mwenye busara hukusanya wakati wa mavuno, kulala wakati wa kuvuna ni aibu.
Methali 10:2-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hazina za uovu hazifaidii kitu; Bali haki huokoa na mauti. BWANA hataiacha nafsi ya mwenye haki ife na njaa; Bali tamaa ya mtu mwovu huisukumia mbali. Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha. Akusanyaye wakati wa joto ni mwana mwenye hekima; Bali asinziaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.
Methali 10:2-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hazina za uovu hazifaidii kitu; Bali haki huokoa na mauti. BWANA hataiacha nafsi ya mwenye haki ife na njaa; Bali tamaa ya mtu mwovu huisukumia mbali. Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha. Akusanyaye wakati wa hari ni mwana mwenye hekima; Bali asinziaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.
Methali 10:2-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hazina zilizopatikana kwa njia mbaya hazifai, lakini uadilifu huokoa kutoka mautini. BWANA hawaachi waadilifu kukaa njaa, lakini hupinga tamaa ya mtu mwovu. Mikono mivivu hufanya mtu kuwa maskini lakini mikono yenye bidii huleta utajiri. Yeye akusanyaye mazao wakati wa kiangazi ni mwana mwenye hekima, lakini yeye alalaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.