Methali 10:17-19
Methali 10:17-19 Biblia Habari Njema (BHN)
Anayekubali maonyo anaelekea kwenye uhai, lakini anayekataa kuonywa amepotoka. Amchukiaye mwingine kwa siri ni mnafiki, anayemsingizia mtu ni mpumbavu. Penye maneno mengi hapakosekani makosa, lakini aneyeuzuia ulimi wake ana busara.
Methali 10:17-19 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Akubaliye kurudiwa huwa katika njia ya uzima; Bali yeye aachaye maonyo hukosa. Yeye afichaye chuki ana midomo ya uongo, Na yeye asingiziaye ni mpumbavu. Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili.
Methali 10:17-19 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Akubaliye kurudiwa huwa katika njia ya uzima; Bali yeye aachaye maonyo hukosa. Yeye afichaye chuki ana midomo ya uongo, Na yeye asingiziaye ni mpumbavu. Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili.
Methali 10:17-19 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Anayekubali kuadibishwa yuko katika njia ya uzima, lakini yeyote anayepuuza maonyo hupotosha wengine. Yeye afichaye chuki yake ana midomo ya uongo, na yeyote anayeeneza uchonganishi ni mpumbavu. Dhambi haiondolewi kwa maneno mengi, bali wenye busara huzuia ulimi wao.