Methali 10:1-3
Methali 10:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Hizi ni methali za Solomoni: Mtoto mwenye hekima ni furaha ya baba yake; lakini mtoto mpumbavu ni huzuni ya mama yake. Mali iliyopatikana kwa njia mbaya haifai, lakini uadilifu huokoa mtu kutoka kifoni. Mwenyezi-Mungu hawaachi waadilifu wapate njaa, lakini huzipinga tamaa za waovu.
Methali 10:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye. Hazina za uovu hazifaidii kitu; Bali haki huokoa na mauti. BWANA hataiacha nafsi ya mwenye haki ife na njaa; Bali tamaa ya mtu mwovu huisukumia mbali.
Methali 10:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye. Hazina za uovu hazifaidii kitu; Bali haki huokoa na mauti. BWANA hataiacha nafsi ya mwenye haki ife na njaa; Bali tamaa ya mtu mwovu huisukumia mbali.
Methali 10:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mithali za Sulemani: Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake, lakini mwana mpumbavu huleta huzuni kwa mama yake. Hazina zilizopatikana kwa njia mbaya hazifai, lakini uadilifu huokoa kutoka mautini. BWANA hawaachi waadilifu kukaa njaa, lakini hupinga tamaa ya mtu mwovu.