Methali 10:1-14
Methali 10:1-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Hizi ni methali za Solomoni: Mtoto mwenye hekima ni furaha ya baba yake; lakini mtoto mpumbavu ni huzuni ya mama yake. Mali iliyopatikana kwa njia mbaya haifai, lakini uadilifu huokoa mtu kutoka kifoni. Mwenyezi-Mungu hawaachi waadilifu wapate njaa, lakini huzipinga tamaa za waovu. Uvivu husababisha umaskini, lakini mkono wa mtu wa bidii hutajirisha. Mwenye busara hukusanya wakati wa mavuno, kulala wakati wa kuvuna ni aibu. Mwadilifu hujiletea baraka yeye mwenyewe, lakini kinywa cha mwovu kimesongwa na ukatili. Waadilifu hukumbukwa kwa baraka, lakini waovu watasahaulika kabisa. Mwenye hekima moyoni hutii amri, lakini mpumbavu aropokaye ataangamia. Aishiye kwa unyofu huishi salama, apotoshaye maisha yake atagunduliwa. Akonyezaye kwa nia mbaya huzusha taabu, lakini aonyaye kwa ujasiri huleta amani. Kinywa cha mwadilifu ni chemchemi ya uhai, lakini kinywa cha mwovu kimesongwa na ukatili. Chuki huzusha ugomvi, lakini upendo hufunika makosa yote. Kinywani mwa mwenye ufahamu mna hekima, lakini wasio na akili watachapwa viboko mgongoni. Wenye hekima huhifadhi maarifa, lakini kuropoka kwa mpumbavu huleta maangamizi haraka.
Methali 10:1-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye. Hazina za uovu hazifaidii kitu; Bali haki huokoa na mauti. BWANA hataiacha nafsi ya mwenye haki ife na njaa; Bali tamaa ya mtu mwovu huisukumia mbali. Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha. Akusanyaye wakati wa joto ni mwana mwenye hekima; Bali asinziaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha. Baraka humkalia mwenye haki kichwani; Bali jeuri hufunika kinywa chake mtu mwovu. Kuwakumbuka wenye haki huwa na baraka; Bali jina la mtu mwovu litaoza. Aliye na akili moyoni mwake atapokea agizo; Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka. Aendaye kwa unyofu huenda salama; Bali apotoshaye njia zake atajulikana. Akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko; Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka. Kinywa chake mwenye haki ni chemchemi ya uzima; Bali jeuri hufunika kinywa chake mtu mwovu, Kuchukiana huleta fitina; Bali kupendana husitiri makosa yote. Hekima hupatikana midomoni mwa mwenye ufahamu; Bali fimbo hufaa kwa mgongo wake asiye na ufahamu. Watu wenye akili huweka akiba ya maarifa; Bali kinywa cha mpumbavu ni uangamivu ulio karibu.
Methali 10:1-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye. Hazina za uovu hazifaidii kitu; Bali haki huokoa na mauti. BWANA hataiacha nafsi ya mwenye haki ife na njaa; Bali tamaa ya mtu mwovu huisukumia mbali. Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha. Akusanyaye wakati wa hari ni mwana mwenye hekima; Bali asinziaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha. Baraka humkalia mwenye haki kichwani; Bali jeuri hufunika kinywa chake mtu mwovu. Kuwakumbuka wenye haki huwa na baraka; Bali jina la mtu mwovu litaoza. Aliye na akili moyoni mwake atapokea agizo; Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka. Aendaye kwa unyofu huenda salama; Bali apotoshaye njia zake atajulikana. Akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko; Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka. Kinywa chake mwenye haki ni chemchemi ya uzima; Bali jeuri hufunika kinywa chake mtu mwovu, Kuchukiana huondokesha fitina; Bali kupendana husitiri makosa yote. Hekima hupatikana midomoni mwa mwenye ufahamu; Bali fimbo hufaa kwa mgongo wake asiye na ufahamu. Watu wenye akili huweka akiba ya maarifa; Bali kinywa cha mpumbavu ni uangamivu ulio karibu.
Methali 10:1-14 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mithali za Sulemani: Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake, lakini mwana mpumbavu huleta huzuni kwa mama yake. Hazina zilizopatikana kwa njia mbaya hazifai, lakini uadilifu huokoa kutoka mautini. BWANA hawaachi waadilifu kukaa njaa, lakini hupinga tamaa ya mtu mwovu. Mikono mivivu hufanya mtu kuwa maskini lakini mikono yenye bidii huleta utajiri. Yeye akusanyaye mazao wakati wa kiangazi ni mwana mwenye hekima, lakini yeye alalaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha. Baraka huwa taji kichwani mwa mwenye haki, lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu. Kumbukumbu ya mwenye haki itakuwa baraka, lakini jina la mwovu litaoza. Mwenye hekima moyoni hupokea maagizo, lakini mpumbavu apayukaye huangamia. Mtu mwadilifu hutembea salama, lakini mtu aendaye katika njia zilizopotoka atagunduliwa. Yeye akonyezaye kwa nia mbaya husababisha huzuni, naye mpumbavu apayukaye huangamia. Kinywa cha mwenye haki ni chemchemi ya uzima, lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu. Chuki huchochea faraka, lakini upendo husitiri mabaya yote. Hekima hupatikana katika midomo ya wenye kupambanua, lakini fimbo ni kwa ajili ya mgongo wake asiye na ufahamu. Wenye hekima huhifadhi maarifa, bali kinywa cha mpumbavu hualika maangamizi.