Methali 1:7-15
Methali 1:7-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu. Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako, wala usiyapuuze mafundisho ya mama yako; hayo yatakupamba kilemba kichwani pako, kama mkufu shingoni mwako. Mwanangu, usikubali kushawishiwa na wenye dhambi. Wakisema: “Twende tukamvizie mtu na kumuua; njoo tukawashambulie wasio na hatia! Tutawameza kama Kuzimu wakiwa hai, watakuwa kama wale washukao Shimoni. Tutajitwalia mali zote za thamani, nyumba zetu tutazijaza nyara. Njoo ushirikiane nasi, vyote tutakavyopata tutagawana.” Wewe mwanangu usiandamane nao, uzuie mguu wako usifuatane nao.
Methali 1:7-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu. Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako, Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako, Na mikufu shingoni mwako. Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usikubali. Wakisema, Haya! Njoo pamoja nasi, Na tuvizie ili kumwaga damu; Tumwotee asiye na hatia, bila sababu; Tuwameze hai kama kuzimu, Na wazima, kama wao washukao shimoni. Tutapata mali yote ya thamani, Tutazijaza nyumba zetu mateka. Wewe utashirikiana nasi; Tutakuwa na vitu vyote kwa shirika. Mwanangu, usiende njiani pamoja nao; Uzuie mguu wako usiende katika mapito yao.
Methali 1:7-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu. Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako, Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako, Na mikufu shingoni mwako. Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usikubali. Wakisema, Haya! Njoo pamoja nasi, Na tuvizie ili kumwaga damu; Tumwotee asiye na hatia, bila sababu; Tuwameze hai kama kuzimu, Na wazima, kama wao washukao shimoni. Tutapata mali yote ya thamani, Tutazijaza nyumba zetu mateka. Wewe utashirikiana nasi; Tutakuwa na vitu vyote shirika. Mwanangu, usiende njiani pamoja nao; Uzuie mguu wako usiende katika mapito yao.
Methali 1:7-15 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu. Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako, wala usiyaache mafundisho ya mama yako. Hayo yatakuwa taji la maua la neema kichwani pako, na mkufu wa kuipamba shingo yako. Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, usikubaliane nao. Wakisema, “Twende tufuatane; tukamvizie mtu na kumwaga damu, njoo tukavizie nafsi isiyo na hatia; tuwameze wakiwa hai kama kaburi, wakiwa wazima kama wale wanaotumbukia shimoni. Tutapata aina zote za vitu vya thamani na kujaza nyumba zetu kwa nyara. Njoo ushirikiane nasi, vitu vyote tutakavyopata tutagawana.” Mwanangu, usiandamane nao. Usiweke mguu wako katika njia zao