Methali 1:20-33
Methali 1:20-33 Biblia Habari Njema (BHN)
Hekima huita kwa sauti barabarani, hupaza sauti yake sokoni; huita juu ya kuta, hutangaza penye malango ya mji: “Enyi wajinga! Mpaka lini mtapenda kuwa wajinga? Mpaka lini wenye dharau watafurahia dharau zao, na wapumbavu kuchukia maarifa? Sikilizeni maonyo yangu; nitawamiminia mawazo yangu, nitawajulisha maneno yangu. Kwa kuwa nimewaita mkakataa kusikiliza, nimewapungia mkono mje mkakataa, mkapuuza mashauri yangu yote, wala hamkuyajali maonyo yangu, nami pia nitayachekelea maafa yenu, nitawadhihaki mnapokumbwa na hofu, hofu itakapowakumba kama tufani, maafa yenu yatakapowavamia kama kimbunga, wakati udhia na dhiki vitakapowapata. Hapo ndipo mtakaponiita lakini sitaitika; mtanitafuta kwa bidii lakini hamtanipata. Kwa kuwa mliyachukia maarifa, wala hamkuchagua kumcha Mwenyezi-Mungu; maadamu mlikataa shauri langu, mkayapuuza maonyo yangu yote; basi, mtakula matunda ya mienendo yenu, mtavimbiwa kwa hila zenu wenyewe. Maana wajinga hujiua kwa ukaidi wao, wapumbavu hujiangamiza kwa kujiamini kwao. Lakini kila anisikilizaye atakaa salama, atatulia bila kuogopa mabaya.”
Methali 1:20-33 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hekima hulia kwa sauti katika njia kuu, Hupaza sauti yake katika viwanja; Hulia penye mikutano mikubwa ya watu, Mahali pa kuyaingilia malango, Ndani ya mji hutamka maneno yake. Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga? Na wenye dharau kupenda dharau yao, Na wapumbavu kuchukia maarifa? Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu; Tazama, nitawamwagia roho yangu, Na kuwajulisheni maneno yangu. Kwa kuwa nimeita, nanyi mkakataa; Nimeunyosha mkono wangu, wala hakuna aliyeangalia; Bali mmeupuuza ushauri wangu, Wala hamkutaka maonyo yangu; Mimi nami nitacheka siku ya msiba wenu, Nitadhihaki hofu yenu ifikapo; Hofu yenu ifikapo kama tufani, Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli, Dhiki na taabu zitakapowafikia. Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika; Watanitafuta kwa bidii, wasinione. Kwa kuwa walichukia maarifa, Wala hawakuchagua kumcha BWANA. Hawakukubali mashauri yangu, Wakayadharau maonyo yangu yote. Kwa hiyo watakula matunda ya njia yao, Watashiba mashauri yao wenyewe. Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza. Bali kila anisikilizaye atakaa salama, Naye atatulia bila kuogopa mabaya.

Methali 1:20-33 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hekima hupaza sauti yake katika njia kuu, Hutoa sauti yake katika viwanja; Hulia penye mikutano mikubwa ya watu, Mahali pa kuyaingilia malango, Ndani ya mji hutamka maneno yake. Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga? Na wenye dharau kupenda dharau yao, Na wapumbavu kuchukia maarifa? Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu; Tazama, nitawamwagia roho yangu, Na kuwajulisheni maneno yangu. Kwa kuwa nimeita, nanyi mkakataa; Nimeunyosha mkono wangu, asiangalie mtu; Bali mmebatilisha shauri langu, Wala hamkutaka maonyo yangu; Mimi nami nitacheka siku ya msiba wenu, Nitadhihaki hofu yenu ifikapo; Hofu yenu ifikapo kama tufani, Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli, Dhiki na taabu zitakapowafikia. Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika; Watanitafuta kwa bidii, wasinione. Kwa kuwa walichukia maarifa, Wala hawakuchagua kumcha BWANA. Hawakukubali mashauri yangu, Wakayadharau maonyo yangu yote. Kwa hiyo watakula matunda ya njia yao, Watashiba mashauri yao wenyewe. Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza. Bali kila anisikilizaye atakaa salama, Naye atatulia bila kuogopa mabaya.
Methali 1:20-33 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hekima huita kwa sauti kuu barabarani, hupaza sauti yake kwenye viwanja vikubwa; kwenye makutano ya barabara za mji zenye makelele mengi hupaza sauti, kwenye malango ya mji hutoa hotuba yake: “Enyi wajinga, mtashikilia ujinga wenu hadi lini? Hadi lini wenye mizaha watafurahia mizaha, na wapumbavu kuchukia maarifa? Kama mngekuwa mmeitikia karipio langu, ningekuwa nimemimina roho yangu kwenu na kuwafahamisha maneno yangu. Lakini kwa kuwa mlinikataa nilipowaita na hakuna yeyote aliyekubali niliponyoosha mkono wangu, kwa kuwa mliyapuuza mashauri yangu yote na hamkukubali karipio langu, mimi nami nitawacheka katika maafa yenu, nitawadhihaki janga litakapowapata: janga litakapowapata kama tufani, maafa yatakapowazoa kama upepo wa kisulisuli, dhiki na taabu zitakapowalemea. “Ndipo watakaponiita lakini sitawajibu; watanitafuta lakini hawatanipata. Kwa kuwa walichukia maarifa, wala hawakuchagua kumcha BWANA, kwa kuwa hawakukubali mashauri yangu, na kukataa maonyo yangu, watakula matunda ya njia zao, na watashibishwa matunda ya hila zao. Kwa kuwa ukaidi wa wajinga utawaua, na kuridhika kwa wajinga kutawaangamiza. Lakini yeyote anisikilizaye ataishi kwa usalama, atatulia, bila kuwa na hofu ya madhara.”