Methali 1:1-33
Methali 1:1-33 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mithali za Sulemani mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli: Kwa kupata hekima na nidhamu; kwa kufahamu maneno ya busara; kwa kujipatia nidhamu na busara, kufanya lililo sawa, haki na bila kupendelea; huwapa busara wajinga, maarifa na akili kwa vijana; wenye hekima na wasikilize nao waongeze elimu yao, wenye kupambanua na wapate mwongozo; kwa kufahamu mithali na mifano, misemo na vitendawili vya wenye hekima. Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu. Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako, wala usiyaache mafundisho ya mama yako. Hayo yatakuwa taji la maua la neema kichwani pako, na mkufu wa kuipamba shingo yako. Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, usikubaliane nao. Wakisema, “Twende tufuatane; tukamvizie mtu na kumwaga damu, njoo tukavizie nafsi isiyo na hatia; tuwameze wakiwa hai kama kaburi, wakiwa wazima kama wale wanaotumbukia shimoni. Tutapata aina zote za vitu vya thamani na kujaza nyumba zetu kwa nyara. Njoo ushirikiane nasi, vitu vyote tutakavyopata tutagawana.” Mwanangu, usiandamane nao. Usiweke mguu wako katika njia zao, kwa kuwa miguu yao hukimbilia kwenye dhambi, ni wepesi kumwaga damu. Tazama ni jinsi gani ilivyo kazi bure kutandaza wavu wakati ndege wote wanakuona! Watu hawa huvizia kumwaga damu yao wenyewe; hujivizia tu wenyewe! Huu ndio mwisho wa wote ambao wanajipatia mali kwa hila; huuondoa uhai wa wale wenye mali. Hekima huita kwa sauti kuu barabarani, hupaza sauti yake kwenye viwanja vikubwa; kwenye makutano ya barabara za mji zenye makelele mengi hupaza sauti, kwenye malango ya mji hutoa hotuba yake: “Enyi wajinga, mtashikilia ujinga wenu hadi lini? Hadi lini wenye mizaha watafurahia mizaha, na wapumbavu kuchukia maarifa? Kama mngekuwa mmeitikia karipio langu, ningekuwa nimemimina roho yangu kwenu na kuwafahamisha maneno yangu. Lakini kwa kuwa mlinikataa nilipowaita na hakuna yeyote aliyekubali niliponyoosha mkono wangu, kwa kuwa mliyapuuza mashauri yangu yote na hamkukubali karipio langu, mimi nami nitawacheka katika maafa yenu, nitawadhihaki janga litakapowapata: janga litakapowapata kama tufani, maafa yatakapowazoa kama upepo wa kisulisuli, dhiki na taabu zitakapowalemea. “Ndipo watakaponiita lakini sitawajibu; watanitafuta lakini hawatanipata. Kwa kuwa walichukia maarifa, wala hawakuchagua kumcha BWANA, kwa kuwa hawakukubali mashauri yangu, na kukataa maonyo yangu, watakula matunda ya njia zao, na watashibishwa matunda ya hila zao. Kwa kuwa ukaidi wa wajinga utawaua, na kuridhika kwa wajinga kutawaangamiza. Lakini yeyote anisikilizaye ataishi kwa usalama, atatulia, bila kuwa na hofu ya madhara.”
Methali 1:1-33 Biblia Habari Njema (BHN)
Hizi ni methali za Solomoni mfalme wa Israeli, mwana wa Daudi. Methali hizi zawapatia watu hekima na nidhamu; zawafanya waelewe maneno ya busara, zawafanya kuwa na nidhamu, utaratibu, uadilifu, haki na kutenda kwa usawa. Huwapatia wajinga werevu na vijana maarifa na hadhari. Mwenye hekima azisikie na kuongeza elimu yake, naye mwenye busara apate mwongozo. Mtu aelewe methali na mifano, maneno ya wenye hekima na vitendawili vyao. Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu. Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako, wala usiyapuuze mafundisho ya mama yako; hayo yatakupamba kilemba kichwani pako, kama mkufu shingoni mwako. Mwanangu, usikubali kushawishiwa na wenye dhambi. Wakisema: “Twende tukamvizie mtu na kumuua; njoo tukawashambulie wasio na hatia! Tutawameza kama Kuzimu wakiwa hai, watakuwa kama wale washukao Shimoni. Tutajitwalia mali zote za thamani, nyumba zetu tutazijaza nyara. Njoo ushirikiane nasi, vyote tutakavyopata tutagawana.” Wewe mwanangu usiandamane nao, uzuie mguu wako usifuatane nao. Maana wao wako mbioni kutenda maovu, haraka zao zote ni za kumwaga damu. Mtego utegwao huku ndege anaona, mtego huo wategwa bure. Wao huvizia na kujiangamiza wao wenyewe, hutega mtego wa kujinasa wao wenyewe. Ndivyo zilivyo njia za waishio kwa ukatili; ukatili huyaangamiza maisha ya wakatili. Hekima huita kwa sauti barabarani, hupaza sauti yake sokoni; huita juu ya kuta, hutangaza penye malango ya mji: “Enyi wajinga! Mpaka lini mtapenda kuwa wajinga? Mpaka lini wenye dharau watafurahia dharau zao, na wapumbavu kuchukia maarifa? Sikilizeni maonyo yangu; nitawamiminia mawazo yangu, nitawajulisha maneno yangu. Kwa kuwa nimewaita mkakataa kusikiliza, nimewapungia mkono mje mkakataa, mkapuuza mashauri yangu yote, wala hamkuyajali maonyo yangu, nami pia nitayachekelea maafa yenu, nitawadhihaki mnapokumbwa na hofu, hofu itakapowakumba kama tufani, maafa yenu yatakapowavamia kama kimbunga, wakati udhia na dhiki vitakapowapata. Hapo ndipo mtakaponiita lakini sitaitika; mtanitafuta kwa bidii lakini hamtanipata. Kwa kuwa mliyachukia maarifa, wala hamkuchagua kumcha Mwenyezi-Mungu; maadamu mlikataa shauri langu, mkayapuuza maonyo yangu yote; basi, mtakula matunda ya mienendo yenu, mtavimbiwa kwa hila zenu wenyewe. Maana wajinga hujiua kwa ukaidi wao, wapumbavu hujiangamiza kwa kujiamini kwao. Lakini kila anisikilizaye atakaa salama, atatulia bila kuogopa mabaya.”
Methali 1:1-33 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mithali za Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli. Kujua hekima na adabu; kutambua maneno ya ufahamu; kufundishwa matendo ya busara, katika haki na hukumu na adili. Kuwapa wajinga werevu, na kijana maarifa na tahadhari; mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia. Kufahamu mithali na kitendawili, na maneno ya wenye hekima na mafumbo yao. Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu. Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako, Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako, Na mikufu shingoni mwako. Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usikubali. Wakisema, Haya! Njoo pamoja nasi, Na tuvizie ili kumwaga damu; Tumwotee asiye na hatia, bila sababu; Tuwameze hai kama kuzimu, Na wazima, kama wao washukao shimoni. Tutapata mali yote ya thamani, Tutazijaza nyumba zetu mateka. Wewe utashirikiana nasi; Tutakuwa na vitu vyote kwa shirika. Mwanangu, usiende njiani pamoja nao; Uzuie mguu wako usiende katika mapito yao. Maana miguu yao huenda mbio maovuni, Nao hufanya haraka ili kumwaga damu. Kwa kuwa mtego hutegwa bure, Mbele ya macho ya ndege yeyote. Na hao hujiotea damu yao wenyewe, Hujinyemelea nafsi zao wenyewe. Ndivyo zilivyo njia za kila mwenye tamaa ya mali; Huuondoa uhai wao walio nayo. Hekima hulia kwa sauti katika njia kuu, Hupaza sauti yake katika viwanja; Hulia penye mikutano mikubwa ya watu, Mahali pa kuyaingilia malango, Ndani ya mji hutamka maneno yake. Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga? Na wenye dharau kupenda dharau yao, Na wapumbavu kuchukia maarifa? Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu; Tazama, nitawamwagia roho yangu, Na kuwajulisheni maneno yangu. Kwa kuwa nimeita, nanyi mkakataa; Nimeunyosha mkono wangu, wala hakuna aliyeangalia; Bali mmeupuuza ushauri wangu, Wala hamkutaka maonyo yangu; Mimi nami nitacheka siku ya msiba wenu, Nitadhihaki hofu yenu ifikapo; Hofu yenu ifikapo kama tufani, Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli, Dhiki na taabu zitakapowafikia. Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika; Watanitafuta kwa bidii, wasinione. Kwa kuwa walichukia maarifa, Wala hawakuchagua kumcha BWANA. Hawakukubali mashauri yangu, Wakayadharau maonyo yangu yote. Kwa hiyo watakula matunda ya njia yao, Watashiba mashauri yao wenyewe. Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza. Bali kila anisikilizaye atakaa salama, Naye atatulia bila kuogopa mabaya.
Methali 1:1-33 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mithali za Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli. Kujua hekima na adabu; kutambua maneno ya ufahamu; kufundishwa matendo ya busara, katika haki na hukumu na adili. Kuwapa wajinga werevu, na kijana maarifa na hadhari; mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia. Kufahamu mithali na kitendawili, na maneno ya wenye hekima na mafumbo yao. Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu. Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako, Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako, Na mikufu shingoni mwako. Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usikubali. Wakisema, Haya! Njoo pamoja nasi, Na tuvizie ili kumwaga damu; Tumwotee asiye na hatia, bila sababu; Tuwameze hai kama kuzimu, Na wazima, kama wao washukao shimoni. Tutapata mali yote ya thamani, Tutazijaza nyumba zetu mateka. Wewe utashirikiana nasi; Tutakuwa na vitu vyote shirika. Mwanangu, usiende njiani pamoja nao; Uzuie mguu wako usiende katika mapito yao. Maana miguu yao huenda mbio maovuni, Nao hufanya haraka ili kumwaga damu. Kwa kuwa mtego hutegwa bure, Mbele ya macho ya ndege ye yote. Na hao hujiotea damu yao wenyewe, Hujinyemelea nafsi zao wenyewe. Ndivyo zilivyo njia za kila mwenye tamaa ya mali; Huuondoa uhai wao walio nayo. Hekima hupaza sauti yake katika njia kuu, Hutoa sauti yake katika viwanja; Hulia penye mikutano mikubwa ya watu, Mahali pa kuyaingilia malango, Ndani ya mji hutamka maneno yake. Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga? Na wenye dharau kupenda dharau yao, Na wapumbavu kuchukia maarifa? Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu; Tazama, nitawamwagia roho yangu, Na kuwajulisheni maneno yangu. Kwa kuwa nimeita, nanyi mkakataa; Nimeunyosha mkono wangu, asiangalie mtu; Bali mmebatilisha shauri langu, Wala hamkutaka maonyo yangu; Mimi nami nitacheka siku ya msiba wenu, Nitadhihaki hofu yenu ifikapo; Hofu yenu ifikapo kama tufani, Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli, Dhiki na taabu zitakapowafikia. Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika; Watanitafuta kwa bidii, wasinione. Kwa kuwa walichukia maarifa, Wala hawakuchagua kumcha BWANA. Hawakukubali mashauri yangu, Wakayadharau maonyo yangu yote. Kwa hiyo watakula matunda ya njia yao, Watashiba mashauri yao wenyewe. Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza. Bali kila anisikilizaye atakaa salama, Naye atatulia bila kuogopa mabaya.