Obadia 1:3-7
Obadia 1:3-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Kiburi chako kimekudanganya: Kwa kuwa mji wako mkuu ni ngome ya miamba imara na makao yako yapo juu milimani, hivyo wajisemea, ‘Nani awezaye kunishusha chini?’ Hata ukiruka juu kama tai, ukafanya makao yako kati ya nyota, mimi nitakushusha chini tu. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu. “Kama wezi au wanyang'anyi wangekujia usiku, je, wasingechukua tu kiasi cha kuwatosha? Ikiwa wavunaji zabibu wangekujia, je, wasingekuachia kiasi kidogo tu? Lakini wewe, adui zako wamekuangamiza kabisa. Enyi wazawa wa Esau, mali zenu zimetekwa; hazina zenu zote zimeporwa! Washirika wenzenu wamewadanganya, wamewafukuza nchini mwenu. Mliopatana nao wamewashinda vitani, rafiki wa kutegemewa ndio waliokutegea mitego, nawe hukuelewa yaliyokuwa yanatendeka.
Obadia 1:3-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Mwenye makao yako juu sana; Asemaye moyoni, Ni nani atakayenishusha mimi? Ujapopanda juu kama tai, Ijapokuwa kiota chako kimewekwa kati ya nyota, Nitakushusha kutoka huko; asema BWANA. Kama wezi wangekujia, kama wanyang'anyi wangekujia usiku, (jinsi ulivyokatiliwa mbali!) Je! Wasingeiba kiasi cha kuwatosha? Kama wachumao zabibu wangekujia, je! Wasingeacha baadhi ya zabibu, ziokotwe? Jinsi watu wa Esau wanavyotafutwatafutwa! Jinsi hazina zake zilizofichwa zinavyoulizwaulizwa! Watu wote wa mapatano yako Wamekufukuza, hadi mipakani; Wale waliofanya amani nawe Wamekudanganya, na kukushinda; Walao mkate wako wameweka mtego chini yako; Wala hana ufahamu wa hayo ndani yake.
Obadia 1:3-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Mwenye makao yako juu sana; Asemaye moyoni, Ni nani atakayenishusha mimi? Ujapopanda juu kama tai, Ijapokuwa kioto chako kimewekwa kati ya nyota, Nitakushusha kutoka huko; asema BWANA. Kama wevi wangekujilia, kama wanyang’anyi wangekujilia usiku, (jinsi ulivyokatiliwa mbali!) Je! Wasingeiba kiasi cha kuwatosha? Kama wachumao zabibu wangekujilia, je! Wasingeacha baadhi ya zabibu, ziokotwe? Jinsi watu wa Esau wanavyotafutwa-tafutwa! Jinsi hazina zake zilizofichwa zinavyoulizwa-ulizwa! Watu wote wa mapatano yako Wamekufukuza, hata mipakani; Wale waliofanya amani nawe Wamekudanganya, na kukushinda; Walao mkate wako wameweka mtego chini yako; Wala hana ufahamu wa hayo ndani yake.
Obadia 1:3-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, wewe unayeishi katika mapango ya miamba na kufanya makao yako juu, wewe unayejiambia mwenyewe, ‘Ni nani awezaye kunishusha chini?’ Ingawa unapaa juu kama tai na kufanya kiota chako kati ya nyota, nitakushusha chini kutoka huko,” asema BWANA. “Ikiwa wezi wangekuja kwako, ikiwa wanyangʼanyi wangekujia usiku: Lo! Tazama ni maafa kiasi gani yanakungojea: je, si wangeiba tu kiasi ambacho wangehitaji? Kama wachuma zabibu wangekuja kwako, je, wasingebakiza zabibu chache? Lakini tazama jinsi Esau atakavyotekwa, jinsi hazina zake zilizofichwa zitatekwa nyara! Wote ulioungana nao watakufukuza hadi mpakani, rafiki zako watakudanganya na kukushinda, wale wanaokula mkate wako watakutegea mtego, lakini hutaweza kuugundua.