Obadia 1:18
Obadia 1:18 Biblia Habari Njema (BHN)
Wazawa wa Yakobo watakuwa kama moto na wazawa wa Yosefu kama miali ya moto. Watawaangamiza wazawa wa Esau kama vile moto uteketezavyo mabua makavu, asinusurike hata mmoja wao. Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema.
Shirikisha
Soma Obadia 1Obadia 1:18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa muali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaka kati yao, na kuwateketeza; wala hatasalia mtu awaye yote katika nyumba ya Esau; kwa kuwa BWANA amesema hayo.
Shirikisha
Soma Obadia 1Obadia 1:18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa mwali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaka kati yao, na kuwateketeza; wala hatasalia mtu awaye yote katika nyumba ya Esau; kwa kuwa BWANA amesema hayo.
Shirikisha
Soma Obadia 1