Hesabu 8:14-16
Hesabu 8:14-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Hivi ndivyo utakavyowatenga Walawi miongoni mwa Waisraeli wengine ili wawe wangu. Baada ya kuwatakasa Walawi na kuwatoa kama sadaka ya kutikiswa wataingia ili kuhudumu katika hema la mkutano. Hao wametolewa wawe wangu kabisa, badala ya wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli.
Hesabu 8:14-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndivyo utakavyowatenga Walawi na kuwatoa katika wana wa Israeli; na Walawi watakuwa wangu. Kisha baadaye Walawi wataingia ndani, ili wahudumu katika hema ya kukutania; nawe utawatakasa, na kuwasongeza wawe sadaka ya kutikiswa. Kwa kuwa nimepewa kabisa mimi watu hawa kutoka katika wana wa Israeli; badala ya wote wafunguao mimba, maana, wazaliwa wa kwanza wa wana wa Israeli wote, nimewatwaa wawe wangu.
Hesabu 8:14-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndivyo utakavyowatenga Walawi na kuwatoa katika wana wa Israeli; na Walawi watakuwa wangu. Kisha baadaye Walawi wataingia ndani, ili wafanye utumishi wa hema ya kukutania; nawe utawatakasa, na kuwasongeza wawe sadaka ya kutikiswa. Kwa kuwa nimepewa kabisa mimi watu hawa kutoka katika wana wa Israeli; badala ya wote wafunguao mimba, maana, wazaliwa wa kwanza wa wana wa Israeli wote, nimewatwaa wawe wangu.
Hesabu 8:14-16 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kwa njia hii utakuwa umewatenga Walawi kutoka kwa Waisraeli wengine, nao Walawi watakuwa wangu. “Utakapokuwa umekwisha kuwatakasa Walawi na kuwatoa wawe sadaka ya kuinuliwa, watakuja kufanya kazi yao katika Hema la Kukutania. Wao ndio Waisraeli ambao watatolewa kabisa kwangu. Nimewatwaa kama mali yangu mwenyewe badala ya mzaliwa wa kwanza, mzaliwa wa kwanza wa kiume kutoka kwa kila mwanamke Mwisraeli.