Hesabu 6:22-26
Hesabu 6:22-26 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, “Mwambie Aroni na wanawe kwamba hivi ndivyo mtakavyowabariki Waisraeli: Mtawaambia, ‘Mwenyezi-Mungu awabariki na kuwalinda; Mwenyezi-Mungu awaangalie kwa wema, na kuwafadhili; Mwenyezi-Mungu awaoneshe wema wake na kuwapa amani.’
Hesabu 6:22-26 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Hivi ndivyo mtakavyowabariki wana wa Israeli; mtawaambia; BWANA akubariki, na kukulinda; BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; BWANA akuinulie uso wake, na kukupa amani.
Hesabu 6:22-26 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Hivi ndivyo mtakavyowabarikia wana wa Israeli; mtawaambia; BWANA akubarikie, na kukulinda; BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; BWANA akuinulie uso wake, na kukupa amani.
Hesabu 6:22-26 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
BWANA akamwambia Musa, “Mwambie Haruni na wanawe, ‘Hivi ndivyo mtakavyowabariki Waisraeli. Waambieni: “ ‘ “BWANA akubariki na kukulinda; BWANA akuangazie nuru ya uso wake na kukufadhili; BWANA akugeuzie uso wake na kukupa amani.” ’