Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hesabu 33:1-56

Hesabu 33:1-56 Biblia Habari Njema (BHN)

Vifuatavyo ni vituo ambavyo Waisraeli walipiga kambi walipotoka Misri wakiwa katika makundi ya makabila yao chini ya uongozi wa Mose na Aroni. Mose aliandika jina la kila mahali walipopiga kambi, kituo baada ya kituo, kwa agizo la Mwenyezi-Mungu. Waisraeli waliondoka mjini Ramesesi mnamo siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, siku moja baada ya Pasaka ya kwanza. Waliondoka kwa uhodari mkubwa mbele ya Wamisri wote, ambao walikuwa wanawazika wazaliwa wao wa kwanza wa kiume aliowaua Mwenyezi-Mungu; kwani Mwenyezi-Mungu alikuwa ameiadhibu hata miungu yao. Basi, Waisraeli waliondoka Ramesesi, wakapiga kambi yao huko Sukothi. Kutoka Sukothi, walipiga kambi yao huko Ethamu, ukingoni mwa jangwa. Kutoka Ethamu, waligeuka na kurudi hadi Pi-hahirothi, mashariki ya Baal-sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migdoli. Waliondoka Pi-hahirothi, wakapita bahari ya Shamu mpaka jangwa la Ethamu; walisafiri jangwani mwendo wa siku tatu, wakapiga kambi yao Mara. Kutoka Mara, walisafiri hadi Elimu; huko Elimu kulikuwa na chemchemi kumi na mbili za maji na mitende sabini, wakapiga kambi yao mahali hapo. Walisafiri kutoka Elimu, wakapiga kambi yao karibu na bahari ya Shamu. Kutoka Bahari ya Shamu walipiga kambi yao katika jangwa la Sini. Kutoka jangwa la Sini, walipiga kambi yao Dofka. Kutoka Dofka walipiga kambi yao huko Alushi. Kutoka Alushi walipiga kambi yao huko Refidimu, ambapo hapakuwa na maji ya kunywa. Waliondoka Refidimu wakapiga kambi yao katika jangwa la Sinai. Kutoka Sinai walipiga kambi yao huko Kibroth-hataava. Kutoka Kibroth-hataava, walipiga kambi yao huko Haserothi. Kutoka Haserothi, walipiga kambi yao huko Rithma. Kutoka Rithma, walipiga kambi yao huko Rimon-perezi. Kutoka Rimon-perezi, walipiga kambi yao huko Libna. Kutoka Libna walipiga kambi yao Risa. Waliondoka Risa, wakapiga kambi yao huko Kehelatha. Kutoka Kehelatha, walipiga kambi yao kwenye Mlima Sheferi. Kutoka Mlima Sheferi walipiga kambi yao huko Harada. Kutoka Harada, walipiga kambi yao huko Makelothi. Kutoka Makelothi, walipiga kambi yao huko Tahathi. Kutoka Tahathi walipiga kambi yao Tera. Kutoka Tera walipiga kambi yao Mithka. Kutoka Mithka, walipiga kambi yao Hashmona. Kutoka Hashmona, walipiga kambi yao Moserothi. Kutoka Moserothi, walipiga kambi yao Bene-yaakani. Kutoka Bene-yaakani, walipiga kambi yao Hor-hagidgadi. Kutoka Hor-hagidgadi, walipiga kambi yao Yot-batha. Kutoka Yot-batha, walipiga kambi yao Abrona. Kutoka Abrona, walipiga kambi yao Esion-geberi. Waliondoka Esion-geberi, wakasafiri na kupiga kambi yao katika jangwa la Sini, (yaani Kadeshi). Kutoka Kadeshi, walipiga kambi yao mlimani Hori, mpakani mwa nchi ya Edomu. Kwa agizo la Mwenyezi-Mungu kuhani Aroni alipanda juu ya Mlima Hori, na huko, akafariki mnamo siku ya kwanza ya mwezi wa tano, mwaka wa arubaini tangu Waisraeli walipotoka nchini Misri. Aroni alikuwa na umri wa miaka 123 alipofariki juu ya Mlima Hori. Mfalme wa Aradi, Mkanaani, aliyekaa Negebu katika nchi ya Kanaani, alipata habari kwamba Waisraeli walikuwa wanakuja. Kutoka Mlima Hori, Waisraeli walipiga kambi yao Salmona. Kutoka Salmona, walipiga kambi yao Punoni. Kutoka Punoni, walipiga kambi yao Obothi. Kutoka Obothi, walipiga kambi yao Iye-abarimu, katika eneo la Moabu. Kutoka Iye-abarimu, walipiga kambi yao Dibon-gadi. Kutoka Dibon-gadi, walisafiri na kupiga kambi yao Almon-diblathaimu. Kutoka Almon-diblathaimu, walisafiri na kupiga kambi yao katika milima ya Abarimu, karibu na Mlima Nebo. Kutoka milima ya Abarimu, walisafiri na kupiga kambi yao katika tambarare za Moabu ngambo ya mto Yordani karibu na Yeriko. Walipiga kambi hiyo karibu na mto Yordani kati ya Beth-yeshimothi na bonde la Abel-shitimu kwenye tambarare za Moabu. Katika tambarare za Moabu, ngambo ya mto Yordani karibu na Yeriko, Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, “Waambie Waisraeli kwamba mtakapovuka mto Yordani na kuingia katika nchi ya Kanaani, wafukuzeni wenyeji wote wa nchi hiyo mbele yenu. Mtaziharibu sanamu zao zote za mawe na za kusubu na kupabomoa kila mahali pao pa juu pa ibada. Mtaichukua nchi hiyo na kukaa humo kwa sababu nimewapeni muimiliki. Mtaigawanya nchi hiyo kwa kura kufuata familia zenu; eneo kubwa kwa kabila kubwa na eneo dogo kwa kabila dogo. Lakini kama msipowafukuza wenyeji wa nchi hiyo kwanza, basi wale mtakaowaacha watakuwa kama vibanzi machoni mwenu au miiba kila upande, na watawasumbua. Nami nitawafanyeni nyinyi kama nilivyokusudia kuwafanya wao.”

Shirikisha
Soma Hesabu 33

Hesabu 33:1-56 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Hivi ndivyo vituo vya wana wa Israeli, hapo walipotoka nchi ya Misri kwa vikosi chini ya uongozi wa Musa na Haruni. Musa akaandika jinsi walivyotoka katika vituo, kituo baada ya kituo kwa kufuata amri ya BWANA; na hivi ndivyo vituo: Wakasafiri kutoka Ramesesi mwezi wa kwanza, siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza; siku ya pili baada ya Pasaka, wana wa Israeli wakatoka kwa uhodari mkubwa mbele ya macho ya Wamisri wote, hapo Wamisri walipokuwa wanazika wazaliwa wa kwanza wao wote, BWANA aliokuwa amewapiga kati yao; BWANA akafanya hukumu juu ya miungu yao nayo. Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi, wakapiga kambi katika Sukothi. Kisha wakasafiri kutoka Sukothi, wakapiga kambi Ethamu, palipo katika mwisho wa nyika. Wakasafiri kutoka Ethamu, na kurudi nyuma hata Pi-hahirothi palipokabili Baal-sefoni; wakapiga kambi mbele ya Migdoli. Wakasafiri kutoka hapo mbele ya Hahirothi, wakapita katikati ya bahari na kuingia jangwani; kisha wakaenda safari ya siku tatu katika nyika ya Ethamu, wakapiga kambi Mara. Wakasafiri kutoka Mara, wakafika Elimu; huko Elimu palikuwa na chemchemi za maji kumi na mbili, na mitende sabini; nao wakapiga kambi Elimu. Wakasafiri kutoka Elimu wakapiga kambi karibu na Bahari ya Shamu. Wakasafiri kutoka Bahari ya Shamu, wakapiga kambi katika nyika ya Sini. Wakasafiri kutoka nyika ya Sini, wakapiga kambi Dofka. Wakasafiri kutoka Dofka, wakapiga kambi Alushi. Wakasafiri kutoka Alushi, wakapiga kambi Refidimu, ambapo hapakuwa na maji ya watu kunywa. Wakasafiri kutoka Refidimu, wakapiga kambi katika nyika ya Sinai. Wakasafiri kutoka nyika ya Sinai, wakapiga kambi Kibroth-hataava. Wakasafiri kutoka Kibroth-hataava, wakapiga kambi Haserothi. Wakasafiri kutoka Haserothi, wakapiga kambi Rithma. Wakasafiri kutoka Rithma, wakapiga kambi Rimon-peresi. Wakasafiri kutoka Rimon-peresi, wakapiga kambi Libna. Wakasafiri kutoka Libna, wakapiga kambi Risa. Wakasafiri kutoka Risa, wakapiga kambi Keheletha. Wakasafiri kutoka Keheletha, wakapiga kambi katika mlima wa Sheferi Wakasafiri kutoka huo mlima wa Sheferi, wakapiga kambi Harada. Wakasafiri kutoka Harada, wakapiga kambi Makelothi. Wakasafiri kutoka Makelothi, wakapiga kambi Tahathi. Wakasafiri kutoka Tahathi wakapiga kambi Tera. Wakasafiri kutoka Tera, wakapiga kambi Mithka. Wakasafiri kutoka Mithka, wakapiga kambi Hashmona. Wakasafiri kutoka Hashmona, wakapiga kambi Moserothi. Wakasafiri kutoka Moserothi, wakapiga kambi Bene-yaakani. Wakasafiri kutoka Bene-yaakani, wakapiga kambi Hor-hagidgadi. Wakasafiri kutoka Hor-hagidgadi, wakapiga kambi Yotbatha. Wakasafiri kutoka Yotbatha, wakapiga kambi Abrona. Wakasafiri kutoka Abrona, wakapiga kambi Esion-geberi. Wakasafiri kutoka Esion-geberi, wakapiga kambi katika nyika ya Sini (ni Kadeshi). Wakasafiri kutoka Kadeshi wakapiga kambi katika mlima wa Hori, katika mpaka wa nchi ya Edomu, Haruni akakwea mlima wa Hori, kwa amri ya BWANA, akafa hapo, katika mwaka wa arubaini baada ya wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri, mwezi wa tano, siku ya kwanza ya mwezi. Naye Haruni alikuwa mtu wa umri wa miaka mia moja ishirini na mitatu hapo alipokufa katika mlima wa Hori. Ndipo Mkanaani, mfalme wa Aradi, aliyekaa pande za Negebu katika nchi ya Kanaani akasikia habari za kuja kwao wana wa Israeli. Nao wakasafiri kutoka mlima wa Hori, wakapiga kambi Salmona. Wakasafiri kutoka Salmona, wakapiga kambi Punoni. Wakasafiri kutoka Punoni, wakapiga kambi Obothi. Wakasafiri kutoka Obothi, wakapiga kambi Lye-abarimu, katika mpaka wa Moabu. Wakasafiri kutoka Iye-abarimu, wakapiga kambi Dibon-gadi. Wakasafiri kutoka Dibon-gadi, wakapiga kambi Almon-diblathaimu. Wakasafiri kutoka Almon-diblathaimu, wakapiga kambi katika milima ya Abarimu, kukabili Nebo. Wakasafiri kutoka hiyo milima ya Abarimu, wakapiga kambi katika nchi tambarare za Moabu, karibu na mto wa Yordani, hapo Yeriko. Wakapiga kambi karibu na Yordani, tangu Beth-yeshimothi hata kufikia Abel-shitimu katika nchi tambarare za Moabu. Kisha BWANA akanena na Musa hapo katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko, na kumwambia, Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapovuka mto wa Yordani na kuingia nchi ya Kanaani, ndipo mtakapowafukuza wenyeji wote wa hiyo nchi mbele yenu, nanyi mtayaharibu mawe yao yote yenye kuchorwa sanamu, na kuziharibu sanamu zao zote za kusubu, kuvunjavunja mahali pao pote palipoinuka; nanyi mtaishika hiyo nchi kuimiliki na kuishi humo; kwa kuwa mimi nimewapa ninyi hiyo nchi ili mwimiliki. Nanyi mtairithi nchi kwa kufanya kura, kama jamaa zenu zilivyo; hao walio wengi mtawapa urithi zaidi, na hao waliopunguka utawapa kama kupunguka kwao; mahali popote kura itakapomwangukia mtu yeyote, mahali hapo ni pake; mtarithi kama makabila ya baba zenu yalivyo. Lakini kama hamtaki kuwafukuza wenyeji wa nchi watoke mbele yenu; ndipo hao ambao mtawabakiza watakuwa kama sindano machoni mwenu, na kama miiba ubavuni mwenu, nao watawasumbua katika hiyo nchi ambayo mwakaa. Kisha itakuwa, kama nilivyoazimia kuwatenda wao, ndivyo nitakavyowatenda ninyi.

Shirikisha
Soma Hesabu 33

Hesabu 33:1-56 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Hizi ndizo safari za wana wa Israeli, hapo walipotoka nchi ya Misri kwa jeshi zao chini ya mkono wa Musa na Haruni. Musa akaandika jinsi walivyotoka katika safari zao, kwa amri ya BWANA; na hizi ndizo safari zao kama kutoka kwao kulivyokuwa. Wakasafiri kutoka Ramesesi mwezi wa kwanza, siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza; siku ya pili baada ya Pasaka, wana wa Israeli wakatoka kwa mkono wa nguvu mbele ya macho ya Wamisri wote, hapo Wamisri walipokuwa wanazika wazaliwa wa kwanza wao wote, BWANA aliokuwa amewapiga kati yao; BWANA akafanya hukumu juu ya miungu yao nayo. Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi, wakapanga katika Sukothi. Kisha wakasafiri kutoka Sukothi, wakapanga Ethamu, palipo katika mwisho wa nyika. Wakasafiri kutoka Ethamu, na kurudi nyuma hata Pi-hahirothi palipokabili Baal-sefoni; wakapanga mbele ya Migdoli. Wakasafiri kutoka hapo mbele ya Hahirothi, wakapita katikati ya bahari na kuingia jangwani; kisha wakaenda safari ya siku tatu katika nyika ya Ethamu, wakapanga Mara. Wakasafiri kutoka Mara, wakafikilia Elimu; huko Elimu palikuwa na chemchemi za maji kumi na mbili, na mitende sabini; nao wakapanga hapo. Wakasafiri kutoka Elimu wakapanga karibu na Bahari ya Shamu. Wakasafiri kutoka Bahari ya Shamu, wakapanga katika nyika ya Sini. Wakasafiri kutoka nyika ya Sini, wakapanga Dofka. Wakasafiri kutoka Dofka, wakapanga Alushi. Wakasafiri kutoka Alushi, wakapanga Refidimu, ambapo hapakuwa na maji ya watu kunywa. Wakasafiri kutoka Refidimu, wakapanga katika nyika ya Sinai. Wakasafiri kutoka nyika ya Sinai, wakapanga Kibroth-hataava. Wakasafiri kutoka Kibroth-hataava, wakapanga Haserothi. Wakasafiri kutoka Haserothi, wakapanga Rithma. Wakasafiri kutoka Rithma, wakapanga Rimon-peresi. Wakasafiri kutoka Rimon-peresi, wakapanga Libna. Wakasafiri kutoka Libna, wakapanga Risa. Wakasafiri kutoka Risa, wakapanga Keheletha. Wakasafiri kutoka Keheletha, wakapanga katika mlima wa Sheferi Wakasafiri kutoka huo mlima wa Sheferi, wakapanga Harada. Wakasafiri kutoka Harada, wakapanga Makelothi. Wakasafiri kutoka Makelothi, wakapanga Tahathi. Wakasafiri kutoka Tahathi wakapanga Tera. Wakasafiri kutoka Tera, wakapanga Mithka. Wakasafiri kutoka Mithka, wakapanga Hashmona. Wakasafiri kutoka Hashmona, wakapanga Moserothi. Wakasafiri kutoka Moserothi, wakapanga Bene-yakani. Wakasafiri kutoka Bene-yakani, wakapanga Hor-hagidgadi. Wakasafiri kutoka Hor-hagidgadi, wakapanga Yotbatha. Wakasafiri kutoka Yotbatha, wakapanga Abrona. Wakasafiri kutoka Abrona, wakapanga Esion-geberi. Wakasafiri kutoka Esion-geberi, wakapanga katika nyika ya Sini (ni Kadeshi). Wakasafiri kutoka Kadeshi wakapanga katika mlima wa Hori, katika mpaka wa nchi ya Edomu, Haruni akakwea mlima wa Hori, kwa amri ya BWANA, akafa hapo, katika mwaka wa arobaini baada ya wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri, mwezi wa tano, siku ya kwanza ya mwezi. Naye Haruni alikuwa mtu wa umri wa miaka mia na ishirini na mitatu hapo alipokufa katika mlima wa Hori. Ndipo Mkanaani, mfalme wa Aradi, aliyekaa pande za Negebu katika nchi ya Kanaani akasikia habari za kuja kwao wana wa Israeli. Nao wakasafiri kutoka mlima wa Hori, wakapanga Salmona. Wakasafiri kutoka Salmona, wakapanga Punoni. Wakasafiri kutoka Punoni, wakapanga Obothi. Wakasafiri kutoka Obothi, wakapanga Iye-abarimu, katika mpaka wa Moabu. Wakasafiri kutoka Iye-abarimu, wakapanga Dibon-gadi. Wakasafiri kutoka Dibon-gadi, wakapanga Almon-diblathaimu. Wakasafiri kutoka Almon-diblathaimu, wakapanga katika milima ya Abarimu, kukabili Nebo. Wakasafiri kutoka hiyo milima ya Abarimu, wakapanga katika nchi tambarare za Moabu, karibu na mto wa Yordani, hapo Yeriko. Wakapanga karibu na Yordani, tangu Beth-yeshimothi hata kufikilia Abel-shitimu katika nchi tambarare za Moabu. Kisha BWANA akanena na Musa hapo katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko, na kumwambia, Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapovuka mto wa Yordani na kuingia nchi ya Kanaani, ndipo mtakapowafukuza wenyeji wote wa hiyo nchi mbele yenu, nanyi mtayaharibu mawe yao yote yenye kuchorwa sanamu, na kuziharibu sanamu zao zote za kusubu, kuvunja-vunja mahali pao pote palipoinuka; nanyi mtaishika hiyo nchi kuimiliki na kuketi humo; kwa kuwa mimi nimewapa ninyi hiyo nchi ili mwimiliki. Nanyi mtairithi nchi kwa kufanya kura, kama jamaa zenu zilivyo; hao walio wengi mtawapa urithi zaidi, na hao waliopunguka utawapa kama kupunguka kwao; mahali po pote kura itakapomwangukia mtu ye yote, mahali hapo ni pake; mtarithi kama kabila za baba zenu zilivyo. Lakini kama hamtaki kuwafukuza wenyeji wa nchi watoke mbele yenu; ndipo hao ambao mtakaowasaza watakuwa kama sindano machoni mwenu, na kama miiba ubavuni mwenu, nao watawasumbua katika hiyo nchi ambayo mwakaa. Kisha itakuwa, kama nilivyoazimia kuwatenda wao, ndivyo nitakavyowatenda ninyi.

Shirikisha
Soma Hesabu 33

Hesabu 33:1-56 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Hivi ndivyo vituo katika safari ya Waisraeli walipotoka Misri kwa vikosi chini ya uongozi wa Musa na Haruni. Kwa agizo la BWANA, Musa aliweka kumbukumbu ya vituo katika safari yao. Hivi ndivyo vituo katika safari yao: Waisraeli walisafiri kutoka Ramesesi katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, siku iliyofuata Pasaka. Walitembea kwa ujasiri wazi mbele ya Wamisri wote, waliokuwa wakizika wazaliwa wao wa kwanza wote, ambao BWANA alikuwa amewaua kati yao, kwa kuwa BWANA alikuwa ameleta hukumu juu ya miungu yao. Waisraeli waliondoka Ramesesi na kupiga kambi huko Sukothi. Wakaondoka Sukothi na kupiga kambi huko Ethamu, pembeni mwa jangwa. Wakaondoka Ethamu, wakageuka wakarudi Pi-Hahirothi, hadi mashariki mwa Baal-Sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migdoli. Wakaondoka Pi-Hahirothi wakapita katikati ya bahari hadi jangwani, na baada ya kusafiri kwa siku tatu katika Jangwa la Ethamu, walipiga kambi huko Mara. Wakaondoka Mara wakaenda Elimu, mahali ambapo palikuwa na chemchemi kumi na mbili na mitende sabini, huko wakapiga kambi. Wakaondoka Elimu na kupiga kambi kando ya Bahari ya Shamu. Wakaondoka kando ya Bahari ya Shamu na kupiga kambi katika Jangwa la Sini. Wakaondoka katika Jangwa la Sini, wakapiga kambi huko Dofka. Wakaondoka Dofka, wakapiga kambi huko Alushi. Wakaondoka Alushi, wakapiga kambi Refidimu, mahali ambapo hapakuwa na maji ya watu kunywa. Wakaondoka Refidimu na kupiga kambi katika Jangwa la Sinai. Wakaondoka katika Jangwa la Sinai na kupiga kambi huko Kibroth-Hataava. Wakaondoka Kibroth-Hataava na kupiga kambi huko Haserothi. Wakaondoka Haserothi na kupiga kambi huko Rithma. Wakaondoka Rithma na kupiga kambi huko Rimon-Peresi. Wakaondoka Rimon-Peresi na kupiga kambi huko Libna. Wakaondoka Libna na kupiga kambi huko Risa. Wakaondoka Risa na kupiga kambi huko Kehelatha. Wakaondoka Kehelatha na kupiga kambi kwenye mlima Sheferi. Wakaondoka kwenye mlima Sheferi na kupiga kambi huko Harada. Wakaondoka Harada na kupiga kambi huko Makelothi. Wakaondoka Makelothi na kupiga kambi huko Tahathi. Wakaondoka Tahathi na kupiga kambi huko Tera. Wakaondoka Tera na kupiga kambi huko Mithka. Wakaondoka Mithka na kupiga kambi huko Hashmona. Wakaondoka Hashmona na kupiga kambi Moserothi. Wakaondoka Moserothi na kupiga kambi huko Bene-Yaakani. Wakaondoka Bene-Yaakani na kupiga kambi huko Hor-Hagidgadi. Wakaondoka Hor-Hagidgadi na kupiga kambi huko Yotbatha. Wakaondoka Yotbatha na kupiga kambi huko Abrona. Wakaondoka Abrona na kupiga kambi huko Esion-Geberi. Wakaondoka Esion-Geberi na kupiga kambi huko Kadeshi katika Jangwa la Sini. Wakaondoka Kadeshi na kupiga kambi kwenye Mlima Hori, mpakani mwa Edomu. Kwa amri ya BWANA, kuhani Haruni alipanda Mlima Hori, mahali alipofia katika siku ya kwanza ya mwezi wa tano, mwaka wa arobaini baada ya Waisraeli kutoka Misri. Haruni alikufa juu ya Mlima Hori akiwa na umri wa miaka mia moja ishirini na tatu (123). Mfalme Mkanaani wa Aradi, ambaye aliishi huko Negebu ya Kanaani, akasikia kwamba Waisraeli wanakuja. Wakaondoka kwenye mlima Hori na kupiga kambi huko Salmona. Wakaondoka Salmona, wakapiga kambi huko Punoni. Wakaondoka Punoni, wakapiga kambi huko Obothi. Wakaondoka Obothi, wakapiga kambi huko Iye-Abarimu, mipakani mwa Moabu. Wakaondoka Iye-Abarimu, wakapiga kambi huko Dibon-Gadi. Wakaondoka Dibon-Gadi na kupiga kambi huko Almon-Diblathaimu. Wakaondoka Almon-Diblathaimu na kupiga kambi katika milima ya Abarimu, karibu na Nebo. Wakaondoka kwenye milima ya Abarimu na kupiga kambi kwenye tambarare ya Moabu, kando ya Yordani, ngʼambo ya Yeriko. Huko kwenye tambarare za Moabu walipiga kambi kandokando ya Mto Yordani, kuanzia Beth-Yeshimothi hadi Abel-Shitimu. Katika tambarare za Moabu kando ya Yordani, ngʼambo ya Yeriko, BWANA akamwambia Musa, “Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mtakapovuka Mto Yordani kuingia Kanaani, wafukuzeni wakazi wote wa nchi iliyo mbele yenu. Haribuni sanamu zao zote za kuchongwa, na sanamu zilizotengenezwa kwa kusubu, na kubomoa mahali pao pa juu pa kuabudia. Mtaimiliki nchi hiyo na kukaa huko, kwa kuwa nimewapeni ninyi kuimiliki. Mtaigawanya nchi hiyo kwa kupiga kura, kufuatana na koo zenu. Kwa kundi kubwa zaidi toa urithi mkubwa zaidi, na kwa kundi dogo zaidi urithi mdogo zaidi. Chochote kinachowaangukia kwa kura kitakuwa chao. Mtaigawanya nchi kufuatana na makabila ya babu zenu. “ ‘Lakini kama hamkuwafukuza wenyeji wa nchi hiyo, wale mtakaowaruhusu wabaki watakuwa kama sindano kwenye macho yenu na miiba kwenu kila upande. Watawasumbua katika nchi mtakayoishi. Kisha nitawatenda ninyi kile ambacho nimepanga kuwatenda wao.’ ”

Shirikisha
Soma Hesabu 33