Hesabu 27:18-20
Hesabu 27:18-20 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Mtwae Yoshua mwana wa Nuni, mtu mwenye roho nzuri, kisha umwekee mikono, na kumsimamisha mbele ya kuhani Eleazari na jumuiya yote, umkabidhi jukumu hilo. Mpe sehemu ya mamlaka yako ili jumuiya yote ya Waisraeli imtii.
Hesabu 27:18-20 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA akamwambia Musa, Mtwae Yoshua, mwana wa Nuni, mtu ambaye roho iko ndani yake, ukamwekee mkono wako; kisha ukamweke mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya jumuiya yote; ukampe mausia mbele ya macho yao. Nawe utaweka juu yake sehemu ya heshima yako, ili jumuiya yote ya wana wa Israeli wapate kutii.
Hesabu 27:18-20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA akamwambia Musa, Mtwae Yoshua, mwana wa Nuni, mtu mwenye roho ndani yake, ukamwekee mkono wako; kisha ukamweke mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya mkutano wote; ukampe mausia mbele ya macho yao. Nawe utaweka juu yake sehemu ya heshima yako, ili mkutano wote wa wana wa Israeli wapate kutii.
Hesabu 27:18-20 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kwa hiyo BWANA akamwambia Musa, “Mchukue Yoshua mwana wa Nuni, mtu ambaye Roho yuko ndani yake, uweke mkono juu yake. Msimamishe mbele ya kuhani Eleazari pamoja na kusanyiko lote, umpe maagizo mbele yao. Mpe sehemu ya mamlaka yako ili jumuiya yote ya Waisraeli wapate kumtii.