Hesabu 25:1-18
Hesabu 25:1-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Waisraeli walipokuwa huko Shitimu, wanaume walianza kuzini na wanawake wa Moabu. Wanawake hao waliwaalika Waisraeli washiriki matambiko waliyotambikia miungu yao, nao Waisraeli wakala chakula na kuiabudu miungu yao. Ndivyo Waisraeli walivyojiunga na mungu Baali wa Peori, nayo hasira ya Mwenyezi-Mungu ikawaka dhidi yao. Basi, Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Wachukue viongozi wote wa Israeli, uwanyonge mbele yangu juani, ili ghadhabu yangu dhidi yenu ipite.” Mose akawaambia waamuzi wa Israeli, “Kila mmoja wenu amuue mtu yeyote miongoni mwenu ambaye amejiunga na mungu Baali wa Peori.” Wakati huohuo mtu mmoja akamleta mwanamke mmoja Mmidiani nyumbani kwake, Mose na jumuiya yote ya watu wa Israeli wakiwa wanaomboleza penye lango la hema la mkutano. Basi, Finehasi mwana wa Eleazari mwana wa kuhani Aroni alipoona hayo, aliinuka akatoka katika hiyo jumuiya, akachukua mkuki na kumfuatia yule Mwisraeli mpaka hemani, akawachoma mkuki wote wawili tumboni. Maradhi mabaya yaliyokuwa yamewaangamiza Waisraeli yakakomeshwa. Waliokufa kutokana na maradhi yale mabaya walikuwa watu 24,000. Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa kuhani Aroni, ameizuia hasira yangu dhidi ya Waisraeli; miongoni mwenu ni yeye tu aliyeona wivu kama nilio nao mimi. Ndio maana sikuwaangamiza Waisraeli wote kwa hasira yangu. Kwa hiyo mwambie kwamba ninafanya naye agano la amani. Naagana naye kwamba yeye na wazawa wake watakuwa makuhani milele kwa sababu aliona wivu kwa ajili yangu, Mungu wake, akawafanyia upatanisho Waisraeli.” Huyo Mwisraeli aliyeuawa pamoja na mwanamke wa Kimidiani aliitwa Zimri mwana wa Salu, kiongozi wa jamaa mojawapo katika kabila la Simeoni. Na huyo mwanamke Mmidiani aliyeuawa aliitwa Kozbi binti Suri, aliyekuwa kiongozi wa ukoo fulani huko Midiani. Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Wachokoze Wamidiani na kuwaangamiza, kwa sababu waliwachokoza nyinyi kwa hila zao, wakawadanganya kuhusu jambo la Peori, na kwa sababu ya Kozbi, binti yao, aliyeuawa wakati maradhi mabaya yalipozuka kule Peori.”
Hesabu 25:1-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu; kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao. Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za BWANA zikawaka juu ya Israeli. Kisha BWANA akamwambia Musa, Watwae wakuu wote wa watu hao, uwanyongee juani mbele ya BWANA ili kwamba hizo hasira kali za BWANA ziwaondokee Israeli. Basi Musa akawaambia waamuzi wa Israeli, Waueni kila mtu watu wake waliojiungamanisha na Baal-peori. Na tazama, mtu mmoja miongoni mwa wana wa Israeli akaja na kuwaletea nduguze mwanamke Mmidiani mbele ya macho ya Musa, na mbele ya macho ya mkutano wote wa wana wa Israeli, hapo walipokuwa walia mbele ya mlango wa hema ya kukutania. Naye Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, alipoona jambo hilo, akaondoka hapo katikati ya mkutano, akashika fumo mkononi mwake; akamwandama huyo mtu wa Israeli na kuingia ndani ya hema nyuma yake, naye akawachoma wote wawili kwa fumo lake, yule mume wa Israeli na huyo mwanamke kati ya tumbo lake. Basi pigo likazuiwa kwao wana wa Israeli. Nao waliokufa kwa pigo hilo idadi yao ilikuwa elfu ishirini na nne. Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia, Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, amezigeuza hasira zangu zisiwe juu ya wana Wa Israeli, kwa kuwa alikuwa na wivu kati yao kwa wivu wangu mimi, hata nisiwaangamize wana wa Israeli katika wivu wangu. Basi kwa hiyo, sema, Tazama, nampa yeye agano langu la amani; tena kwake yeye, na kizazi chake baada yake, litakuwa agano la ukuhani wa milele; kwa sababu alikuwa na wivu kwa ajili ya Mungu wake, na kuwafanyia upatanisho wana wa Israeli. Basi jina la Mwisraeli huyo aliyeuawa pamoja na yule mwanamke Mmidiani, aliitwa Zimri, mwana wa Salu, mkuu wa nyumba ya baba zake, katika kabila la Simeoni. Na jina la huyo mwanamke Mmidiani aliyeuawa, aliitwa Kozbi, binti Suri; naye alikuwa kichwa cha watu wa nyumba ya baba zake huko Midiani. Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Wasumbue Wamidiani, na kuwapiga; kwa sababu wao wawasumbua ninyi kwa hila zao, ambazo kwa hizo wamewadanganya ninyi katika jambo la Peori, na katika jambo la huyo Kozbi, binti wa mkuu wa Midiani, dada yao, huyo aliyeuawa siku hiyo ya pigo katika jambo la Peori.
Hesabu 25:1-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu; kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao. Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za BWANA zikawaka juu ya Israeli. Kisha BWANA akamwambia Musa, Watwae wakuu wote wa hao watu, ukamtungikie BWANA watu hao mbele ya jua, ili kwamba hizo hasira kali za BWANA ziwaondokee Israeli. Basi Musa akawaambia waamuzi wa Israeli, Waueni kila mtu watu wake waliojiungamanisha na Baal-peori. Na tazama, mtu mmoja miongoni mwa wana wa Israeli akaja na kuwaletea nduguze mwanamke Mmidiani mbele ya macho ya Musa, na mbele ya macho ya mkutano wote wa wana wa Israeli, hapo walipokuwa walia mbele ya mlango wa hema ya kukutania. Naye Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, alipoona jambo hilo, akaondoka hapo katikati ya mkutano, akashika fumo mkononi mwake; akamwandama huyo mtu wa Israeli na kuingia ndani ya hema nyuma yake, naye akawachoma wote wawili kwa fumo lake, yule mume wa Israeli na huyo mwanamke kati ya tumbo lake. Basi pigo likazuiwa kwao wana wa Israeli. Nao waliokufa kwa hilo pigo walikuwa watu elfu ishirini na nne hesabu yao. Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia, Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, amezigeuza hasira zangu zisiwe juu ya wana Wa Israeli, kwa kuwa alikuwa na wivu kati yao kwa wivu wangu mimi, hata nisiwaangamize wana wa Israeli katika wivu wangu. Basi kwa hiyo, sema, Tazama, nampa yeye agano langu la amani; tena kwake yeye, na kizazi chake baada yake, litakuwa agano la ukuhani wa milele; kwa sababu alikuwa na wivu kwa ajili ya Mungu wake, na kuwafanyia upatanisho wana wa Israeli. Basi jina la Mwisraeli huyo aliyeuawa pamoja na yule mwanamke Mmidiani, aliitwa Zimri, mwana wa Salu, mkuu wa nyumba ya baba zake, katika kabila la Simeoni. Na jina la huyo mwanamke Mmidiani aliyeuawa, aliitwa Kozbi, binti Suri; naye alikuwa kichwa cha watu wa nyumba ya baba zake huko Midiani Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Wasumbue Wamidiani, na kuwapiga; kwa sababu wao wawasumbua ninyi kwa hila zao, ambazo kwa hizo wamewadanganya ninyi katika jambo la Peori, na katika jambo la huyo Kozbi, binti wa mkuu wa Midiani, umbu lao, huyo aliyeuawa siku hiyo ya pigo katika jambo la Peori.
Hesabu 25:1-18 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Israeli alipokuwa akikaa Shitimu, wanaume wa Israeli walianza kuzini na wanawake wa Moabu, ambao waliwaalika kushiriki katika sadaka kwa miungu yao. Watu wakala na kusujudu mbele ya miungu hiyo. Kwa hiyo Israeli akaungana katika kumwabudu Baali wa Peori. Hasira ya BWANA ikawaka dhidi yao. BWANA akamwambia Musa, “Uwachukue viongozi wote wa watu hawa, uwaue hadharani mbele za BWANA, ili hasira kali ya BWANA iweze kuondoka kwa Israeli.” Kwa hiyo Musa akawaambia waamuzi wa Israeli, “Kila mmoja wenu lazima awaue wale wanaume wenu, walioshiriki katika kumwabudu Baali wa Peori.” Ndipo mwanaume Mwisraeli akamleta mwanamke Mmidiani katika jamaa yake palepale mbele ya Musa na mkutano wote wa Israeli walipokuwa wakilia kwenye lango la Hema la Kukutania. Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa kuhani Haruni, alipoona jambo hili, akaondoka kwenye kusanyiko, akachukua mkuki mkononi mwake, akamfuata yule Mwisraeli ndani ya hema. Akawachoma mkuki wote wawili kwa pamoja, ukapenya kwenye mwili wa yule Mwisraeli na mwili wa yule mwanamke. Ndipo tauni dhidi ya Waisraeli ikakoma. Lakini wale waliokufa kwa hiyo tauni walikuwa watu elfu ishirini na nne. BWANA akamwambia Musa, “Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa kuhani Haruni, amegeuza hasira yangu mbali na Waisraeli, kwa sababu alikuwa na wivu kama nilio nao kwa heshima yangu miongoni mwao, hata kwamba kwa wivu wangu sikuwaangamiza. Kwa hiyo mwambie Finehasi ninafanya agano langu la amani naye. Yeye pamoja na wazao wake watakuwa na agano la ukuhani milele, kwa sababu alikuwa na wivu kwa ajili ya heshima ya Mungu wake, na akafanya upatanisho kwa Waisraeli.” Jina la Mwisraeli ambaye aliuawa pamoja na mwanamke Mmidiani ni Zimri mwana wa Salu, kiongozi wa jamaa ya Simeoni. Jina la mwanamke Mmidiani aliyeuawa ni Kozbi binti Suri, aliyekuwa mkuu wa kabila la jamaa ya Wamidiani. BWANA akamwambia Musa, “Watendeeni Wamidiani kama adui na mwaue, kwa sababu wao waliwatendea kama adui wakati waliwadanganya katika tukio la Peori na dada yao Kozbi, binti ya kiongozi Mmidiani, mwanamke ambaye aliuawa wakati tauni ilikuja kama matokeo ya tukio la Peori.”