Hesabu 19:20-22
Hesabu 19:20-22 Biblia Habari Njema (BHN)
“Lakini mtu akiwa najisi asipojitakasa, mtu huyo atakataliwa mbali na jumuiya, kwa kuwa analitia najisi hema la Mwenyezi-Mungu. Kwa vile hakunyunyiziwa maji ya utakaso, yu unajisi. Watu watalishika sharti hili daima. Mtu atakayenyunyiza maji ya kutakasia ataosha nguo zake; naye anayegusa maji hayo ya najisi atakuwa najisi hadi jioni. Chochote atakachogusa mtu najisi kitakuwa najisi, na yeyote atakayekigusa kitu hicho atakuwa najisi mpaka jioni.”
Hesabu 19:20-22 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini mtu atakayekuwa najisi, naye hataki kujitakasa, mtu huyo atakatiliwa mbali katika mkutano, kwa sababu amepatia unajisi mahali patakatifu pa BWANA; hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake; yeye yuko najisi. Nayo itakuwa amri ya siku zote kwao; na yeye anyunyizaye maji ya farakano atazifua nguo zake; naye ayagusaye hayo maji ya farakano atakuwa najisi hadi jioni. Na kitu chochote atakachokigusa mtu aliye najisi kitakuwa najisi; na mtu atakayekigusa kitu hicho atakuwa najisi hadi jioni.
Hesabu 19:20-22 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini mtu atakayekuwa najisi, naye hataki kujitakasa, mtu huyo atakatiliwa mbali katika mkutano, kwa sababu amepatia unajisi mahali patakatifu pa BWANA; hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake; yeye yu najisi. Nayo itakuwa amri ya sikuzote kwao; na yeye anyunyizaye maji ya farakano atazifua nguo zake; naye ayagusaye hayo maji ya farakano atakuwa najisi hata jioni. Na kitu cho chote atakachokigusa mtu aliye najisi kitakuwa najisi; na mtu atakayekigusa kitu hicho atakuwa najisi hata jioni.
Hesabu 19:20-22 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Lakini ikiwa mtu ambaye ni najisi hakujitakasa mwenyewe, ni lazima akatiliwe mbali na jumuiya, kwa sababu ameinajisi Maskani ya BWANA. Maji ya utakaso hayajanyunyizwa juu yake, naye ni najisi. Hili ni agizo la kudumu kwao. “Mtu anayenyunyiza yale maji ya utakaso lazima pia afue nguo zake, na yeyote anayegusa maji ya utakaso atakuwa najisi hadi jioni. Kitu chochote anachogusa mtu aliye najisi kitakuwa najisi, na yeyote akigusaye huwa najisi hadi jioni.”