Hesabu 17:7-8
Hesabu 17:7-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Mose akaziweka fimbo hizo zote mbele ya Mwenyezi-Mungu katika hema la mkutano. Kesho yake asubuhi, Mose alikwenda katika hema la mkutano. Humo, aliikuta fimbo ya Aroni wa kabila la Lawi, imechipua na kutoa vichipukizi vilivyochanua maua na kuzaa matunda mabivu ya mlozi.
Hesabu 17:7-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha Musa akaziweka hizo fimbo mbele za BWANA katika hema ya kukutania. Ilikuwa siku ya pili yake, Musa akaingia ndani ya hema ya ushahidi; na tazama, ile fimbo ya Haruni iliyokuwa kwa nyumba ya Lawi ilikuwa imechipuka, imetoa michipukizi, na kuchanua maua; na kuzaa matunda mabivu.
Hesabu 17:7-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha Musa akaziweka hizo fimbo mbele za BWANA katika hema ya kukutania. Ilikuwa siku ya pili yake, Musa akaingia ndani ya hema ya ushahidi; na tazama, ile fimbo ya Haruni iliyokuwa kwa nyumba ya Lawi ilikuwa imechipuka, imetoa michipukizi, na kuchanua maua; na kuzaa malozi mabivu.
Hesabu 17:7-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Musa akaziweka hizo fimbo mbele za BWANA ndani ya Hema la Ushuhuda. Siku iliyofuata Musa aliingia kwenye Hema la Ushuhuda akaona ile fimbo ya Haruni ambayo iliwakilisha jamaa ya Lawi haikuwa tu imechipuka, bali pia ilikuwa imetoa machipukizi, kuchanua maua na kuzaa malozi.