Hesabu 13:3-6
Hesabu 13:3-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Basi, kwa mujibu wa agizo la Mwenyezi-Mungu, Mose akatuma watu kutoka jangwa la Parani. Watu wote waliotumwa walikuwa viongozi wa makabila mbalimbali ya wana wa Israeli. Ifuatayo ndiyo orodha ya majina ya watu hao: Kabila la Reubeni, Shamua mwana wa Zakuri. Kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori. Kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune.
Hesabu 13:3-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi Musa akawatuma kutoka nyika ya Parani kama alivyoagizwa na BWANA; wote walikuwa ni watu walio vichwa vya wana wa Israeli. Na majina yao ni haya; katika kabila la Reubeni, Shamua mwana Zakuri. Katika kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori. Katika kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune.
Hesabu 13:3-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi Musa akawatuma kutoka nyika ya Parani kama alivyoagizwa na BWANA; wote walikuwa ni watu walio vichwa vya wana wa Israeli. Na majina yao ni haya; katika kabila ya Reubeni, Shamua mwana Zakuri. Katika kabila ya Simeoni, Shafati mwana wa Hori. Katika kabila ya Yuda, Kalebu mwana wa Yefune.
Hesabu 13:3-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hivyo kwa agizo la BWANA Musa akawatuma kutoka Jangwa la Parani. Wote walikuwa viongozi wa Waisraeli. Haya ndiyo majina yao: kutoka kabila la Reubeni, Shamua mwana wa Zakuri; kutoka kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori; kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune