Hesabu 12:5-9
Hesabu 12:5-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Hapo Mwenyezi-Mungu akashuka katika nguzo ya wingu, akasimama kwenye mlango wa hema, akawaita Aroni na Miriamu. Wote wawili wakasogea mbele. Kisha Mwenyezi-Mungu akawaambia, “Sikilizeni maneno yangu: Kama kuna nabii miongoni mwenu, mimi Mwenyezi-Mungu hujifahamisha kwake katika maono na kuongea naye katika ndoto. Lakini kumhusu mtumishi wangu Mose, hali ni tofauti kabisa. Yeye ana jukumu la kuwatunza watu wangu wote. Mimi huongea naye ana kwa ana, waziwazi na si kwa kutumia mafumbo. Yeye huliona umbo langu mimi Mwenyezi-Mungu. Kwa nini, basi, hamkuogopa kusema vibaya dhidi ya mtumishi wangu Mose?” Hapo Mwenyezi-Mungu akawaka hasira dhidi yao, akaondoka, akaenda zake.
Hesabu 12:5-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili. Kisha akawaambia, Sikilizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, BWANA, nitajifunua kwake katika maono, Nitasema naye katika ndoto. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la BWANA yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumteta mtumishi wangu, huyo Musa? Hasira za BWANA zikawaka juu yao; kisha akaenda zake.
Hesabu 12:5-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili. Kisha akawaambia, Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, BWANA, nitajifunua kwake katika maono, Nitasema naye katika ndoto. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la BWANA yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa? Hasira za BWANA zikawaka juu yao; naye akaenda zake.
Hesabu 12:5-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kisha BWANA akashuka katika nguzo ya wingu, akasimama kwenye ingilio la Hema, akawaita Haruni na Miriamu. Waliposogea mbele, BWANA akawaambia, “Sikilizeni maneno yangu: “Akiwepo nabii wa BWANA miongoni mwenu, nitajifunua kwake kwa maono, nitanena naye katika ndoto. Lakini sivyo kwa mtumishi wangu Musa; yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote. Kwake nitanena naye uso kwa uso, waziwazi wala si kwa mafumbo; yeye ataona umbo la BWANA. Kwa nini basi ninyi hamkuogopa kuzungumza kinyume cha mtumishi wangu Musa?” Hasira ya BWANA ikawaka dhidi yao, akawaacha.