Hesabu 12:13-15
Hesabu 12:13-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Mose akamlilia Mwenyezi-Mungu akisema, “Nakusihi, ee Mungu, umponye.” Lakini Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Kama baba yake angemtemea mate usoni, je, hangeaibika kwa siku saba? Basi, mtoe nje ya kambi akae huko muda wa siku saba, kisha unaweza kumruhusu arudi kambini.” Kwa hiyo, Miriamu akafukuzwa nje ya kambi kwa muda wa siku saba. Watu hawakuanza tena safari hadi Miriamu aliporudishwa tena kambini.
Hesabu 12:13-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Musa akamlilia BWANA, akasema, Mponye, Ee Mungu, nakusihi sana. BWANA akamwambia Musa, Je! Kama baba yake angalimtemea mate usoni tu, hangaliona aibu muda wa siku saba? Na afungwe nje ya kambi muda wa siku saba, kisha baada ya hayo ataletwa ndani tena. Basi Miriamu alifungwa nje ya kambi muda wa siku saba; wala watu hawakusafiri hata Miriamu alipoletwa ndani tena.
Hesabu 12:13-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Musa akamlilia BWANA, akasema, Mpoze, Ee Mungu, nakusihi sana. BWANA akamwambia Musa, Je! Kama baba yake angalimtemea mate usoni tu, hangaliona aibu muda wa siku saba? Na afungwe nje ya kambi muda wa siku saba, kisha baada ya hayo ataletwa ndani tena. Basi Miriamu alifungwa nje ya kambi muda wa siku saba; wala watu hawakusafiri hata Miriamu alipoletwa ndani tena.
Hesabu 12:13-15 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hivyo Musa akamlilia BWANA akisema, “Ee Mungu, nakuomba umponye!” BWANA akamjibu Musa, “Je, kama baba yake angemtemea usoni, asingeona aibu kwa siku saba? Mfungie nje ya kambi kwa siku saba; baada ya hapo anaweza kurudishwa kambini.” Kwa hiyo Miriamu akafungiwa nje ya kambi kwa siku saba, nao watu hawakuendelea na safari hadi aliporudishwa kambini.