Hesabu 12:1-3
Hesabu 12:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha Miriamu na Aroni walianza kumsema vibaya Mose kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa. Wakasema, “Hivi kwani Mwenyezi-Mungu amezungumza kwa kumwagiza Mose peke yake? Je, hajazungumza nasi pia?” Mwenyezi-Mungu aliyasikia maneno hayo. (Mose alikuwa mtu mnyenyekevu kuliko watu wengine wote waliokuwa duniani.)
Hesabu 12:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha Miriamu na Haruni wakamteta Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi. Wakasema, Je! Ni kweli BWANA amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? BWANA akasikia maneno yao. Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.
Hesabu 12:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi. Wakasema, Je! Ni kweli BWANA amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? BWANA akasikia maneno yao. Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.
Hesabu 12:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Miriamu na Haruni walianza kuzungumza dhidi ya Musa kwa sababu ya mke wake Mkushi, kwa kuwa alikuwa ameoa Mkushi. Waliuliza, “Je, BWANA amesema kupitia Musa peke yake? Je, hajasema kutupitia sisi pia?” Naye BWANA akasikia hili. (Basi Musa alikuwa mtu mnyenyekevu sana, mnyenyekevu kuliko mtu mwingine yeyote katika uso wa dunia.)