Hesabu 11:1-3
Hesabu 11:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Watu walianza kumlalamikia Mwenyezi-Mungu juu ya taabu zao. Mwenyezi-Mungu aliposikia, alishikwa na hasira, akawapelekea moto. Moto huo uliwaka kati yao na kuchoma upande mmoja wa kambi. Watu wakamlilia Mose, naye akamwomba Mwenyezi-Mungu na moto huo ukazimika. Kwa hiyo, mahali hapo pakaitwa Tabera, kwa sababu hapo moto wa Mwenyezi-Mungu uliwaka kati ya watu.
Hesabu 11:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha hao watu walikuwa kama wanung'unikao, wakinena maovu masikioni mwa BWANA; BWANA aliposikia hayo, hasira zake zikawaka; na moto wa BWANA ukawaka kati yao, ukateketeza hadi viunga vya kambi. Ndipo watu wakamlilia Musa; naye Musa akamwomba BWANA, na ule moto ukakoma. Jina la mahali hapo likaitwa Tabera kwa sababu huo moto wa BWANA ukawaka kati yao.
Hesabu 11:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha hao watu walikuwa kama wanung’unikao, wakinena maovu masikioni mwa BWANA; BWANA aliposikia hayo, hasira zake zikawaka; na moto wa BWANA ukawaka kati yao, ukateketeza katika mipaka ya mwisho wa marago. Ndipo watu wakamlilia Musa; naye Musa akamwomba BWANA, na ule moto ukakoma. Jina la mahali hapo likaitwa Tabera; kwa sababu huo moto wa BWANA ukawaka kati yao.
Hesabu 11:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Basi watu wakalalamika kwa habari ya taabu zao masikioni mwa BWANA, naye alipowasikia, hasira yake ikawaka. Ndipo moto kutoka kwa BWANA ukawaka miongoni mwao na kuteketeza baadhi ya viunga vya kambi. Watu walipomlilia Musa, akamwomba BWANA, nao moto ukazimika. Hivyo mahali pale pakaitwa Tabera, kwa sababu moto kutoka kwa BWANA uliwaka miongoni mwao.