Nehemia 7:3
Nehemia 7:3 Biblia Habari Njema (BHN)
nikawaagiza, “Malango yasifunguliwe usiku kucha hadi jua linapokuwa limepanda. Kabla hawajaondoka walinzi ni lazima kufunga milango yote kwa makomeo yake. Teueni walinzi miongoni mwa wakazi wa mji wa Yerusalemu, kila mmoja awe mahali pake kukabiliana na nyumba yake.”
Nehemia 7:3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nikawaambia, Yasifunguliwe malango ya Yerusalemu kabla jua halijachomoza; na kabla walinzi hawajaondoka waifunge milango, mkaikaze; kisha wekeni walinzi wa zamu wa hao wakaao Yerusalemu, kila mtu na zamu yake, na kila mtu kuielekea nyumba yake.
Nehemia 7:3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nikawaambia, Yasifunguliwe malango ya Yerusalemu kabla halijachomoza jua; nao walinzi wangali wakisimama bado, waifunge milango, mkaikaze; kisha wekeni walinzi wa zamu wa hao wakaao Yerusalemu, kila mtu na zamu yake, na kila mtu kuielekea nyumba yake.
Nehemia 7:3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nikawaambia, “Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe hadi jua litakapokuwa limepanda. Walinzi wa malango wakiwa bado kwenye zamu, waamuru wafunge milango na waweke makomeo. Pia wateueni wenyeji wa Yerusalemu wawe walinzi, kila mmoja kwenye lindo lake, na wengine karibu na nyumba zao wenyewe.”