Nehemia 7:1-72
Nehemia 7:1-72 Biblia Habari Njema (BHN)
Baada ya ukuta kukamilika, malango yote kuwa tayari, na kuteuliwa kwa walinzi, waimbaji na Walawi, nilimteua ndugu yangu Hanani kuwa mwangalizi wa Yerusalemu akishirikiana na Hanania aliyekuwa mkuu wa ngome katika Yerusalemu; kwa sababu alikuwa mtu wa kutegemewa na anayemcha sana Mungu, hapakuwapo mwingine aliyelingana naye, nikawaagiza, “Malango yasifunguliwe usiku kucha hadi jua linapokuwa limepanda. Kabla hawajaondoka walinzi ni lazima kufunga milango yote kwa makomeo yake. Teueni walinzi miongoni mwa wakazi wa mji wa Yerusalemu, kila mmoja awe mahali pake kukabiliana na nyumba yake.” Mji wa Yerusalemu ulikuwa mpana na mkubwa, lakini wakazi wake walikuwa wachache na nyumba zilikuwa hazijajengwa. Mungu akanipa moyo kuwakusanya viongozi na watu ili kujua koo zao. Nikapata kitabu cha koo za watu waliorudi toka uhamishoni mara ya kwanza, na hawa wafuatao ndio waliokuwa wameorodheshwa ndani yake. Wale waliokuwa uhamishoni kule Babuloni, walirudi mjini Yerusalemu na nchini Yuda, kila mmoja akarudi mjini kwake. Jamaa zao walikuwa wamekaa Babuloni tangu mfalme Nebukadneza alipowahamishia huko wakiwa mateka. Waliporudi waliongozwa na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Azaria, Raamia, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Misperethi, Bigwai, Nehumu na Baana. Ifuatayo ni idadi ya watu wa koo za Israeli waliorudi toka uhamishoni: Watu wa ukoo wa Paroshi: 2,172; wa ukoo wa Shefatia: 372; wa ukoo wa Ara: 652; wa ukoo wa Pahath-moabu, yaani wazawa wa Yeshua na Yoabu: 2,818; wa ukoo wa Elamu: 1,254; wa ukoo wa Zatu: 845; wa ukoo wa Zakai: 760; wa ukoo wa Binui: 648; wa ukoo wa Bebai: 624; wa ukoo wa Azgadi: 2,322; wa ukoo wa Adonikamu: 667; wa ukoo wa Bigwai: 2,067; wa ukoo wa Adini: 655; wa ukoo wa Ateri (ambao pia unaitwa Hezekia): 98; wa ukoo wa Hashumu: 328; wa ukoo wa Bezai: 324; wa ukoo wa Harifu: 112; wa ukoo wa Gibeoni: 95; Watu wa miji ifuatayo pia walirudi: Wa mji wa Bethlehemu na Netofa: 188; wa mji wa Anathothi: 128; wa mji wa Beth-azmawethi: 42; wa miji ya Kiriath-yearimu, Kefira na Beerothi: 743; wa miji ya Rama na Geba: 621; wa mji wa Mikmashi: 122; wa miji ya Betheli na Ai: 123; wa mji mwingine wa Nebo: 52; wa mji mwingine wa Elamu: 1,254; wa mji wa Harimu: 320; wa mji wa Yeriko: 345; wa miji ya Lodi, Hadidi na Ono: 721; wa mji wa Senaa: 3,930. Ifuatayo ni idadi ya makuhani waliorudi kutoka uhamishoni: Makuhani wa ukoo wa Yedaya, waliokuwa wazawa wa Yeshua: 973; wa ukoo wa Imeri: 1,052; wa ukoo wa Pashuri: 1247; wa ukoo wa Harimu: 1017. Walawi wa ukoo wa Yeshua, yaani Kadmieli, wazawa wa Hodavia waliorudi kutoka uhamishoni walikuwa 74. Waimbaji: Wazawa wa Asafu walikuwa 148. Walinzi: Wazawa wa Shalumu, wa Ateri, wa Talmoni, wa Akubu, wa Hatita na wa Shobai, walikuwa 138. Koo za wahudumu hekaluni waliorudi kutoka uhamishoni zilikuwa: Ukoo wa Ziha, wa Hasufa, wa Tabaothi; wa Kerosi, wa Siaha, wa Padoni; wa Lebana, wa Hagaba, wa Shalmai; wa Hanani, wa Gideli, wa Gahari; wa Reaya, wa Resini, wa Nekoda; wa Gazamu, wa Uza, wa Pasea; wa Besai, wa Meunimu, wa Nefushesimu; wa Bakbuki, wa Hakufa, wa Harhuri; wa Baslithi, wa Mehida, wa Harsha; wa Barkosi, wa Sisera, wa Tema; wa Nezia na ukoo wa Hatifa. Koo za wazawa wa watumishi wa mfalme Solomoni waliorudi kutoka uhamishoni zilikuwa: Ukoo wa Sotai, wa Soferethi, wa Perida; wa Yaala, wa Darkoni, wa Gideli; ukoo wa Shefatia, wa Hatili, wa Pokereth-hasebaimu na ukoo wa Amoni. Basi wahudumu wote wa hekalu na wazawa wa watumishi wa Solomoni, waliorudi kutoka uhamishoni, walikuwa 392. Watu wa miji ifuatayo, nao walirudi: Wa Tel-mela, wa Tel-harsha, wa Kerubu, wa Adoni na wa Imeri; ila haikuwezekana kuthibitisha kama walikuwa wazawa wa Waisraeli wazawa wa Delaya, Tobia na wa Nekoda; jumla: Watu 642. Wazawa wa koo zifuatazo za makuhani pia walirudi: Ukoo wa Hobaya, wa Hakozi na wa Barzilai (aliyekuwa ameoa binti za Barzilai, Mgileadi, naye akachukua jina la ukoo huo). Hao walitafuta orodha yao kati ya wengine walioorodheshwa katika kumbukumbu za koo, lakini ukoo wao haukuwemo. Kwa hiyo hawakuruhusiwa kutiwa katika huduma ya ukuhani kwani walihesabiwa kuwa najisi. Mtawala akawaambia kuwa hawaruhusiwi kushiriki chakula kitakatifu sana, mpaka afike kuhani mwenye kauli ya Urimu na Thumimu. Watu wote waliorudi kutoka uhamishoni jumla yao ilikuwa 42,360. Tena kulikuwa na watumishi wanaume na wanawake 7,337, nao walikuwa waimbaji wanaume na wanawake, wote 245. Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245, ngamia 435, na punda 6,720. Baadhi ya wakuu wa koo walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala wa mkoa alitoa kilo 8 za dhahabu, mabirika 50, mavazi 530. Baadhi ya wakuu wa koo walitoa kilo 168 za dhahabu, na kilo 1,250 za fedha. Matoleo ya watu wengine wote yalikuwa kilo 168 za dhahabu, kilo 140 za fedha na mavazi ya makuhani 67.
Nehemia 7:1-72 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ikawa, baada ya ukuta kujengwa, na milango kuisimamishwa na kuweka mabawabu, waimbaji na Walawi, ndipo nilimteua ndugu yangu Hanani, kuwa mwangalizi wa Yerusalemu akisaidiana na Hanania, jemadari wa ngome, kwa maana alikuwa mtu mwaminifu na mwenye kumcha Mungu kuliko wengi. Nikawaambia, Yasifunguliwe malango ya Yerusalemu kabla jua halijachomoza; na kabla walinzi hawajaondoka waifunge milango, mkaikaze; kisha wekeni walinzi wa zamu wa hao wakaao Yerusalemu, kila mtu na zamu yake, na kila mtu kuielekea nyumba yake. Basi mji ulikuwa wa nafasi nyingi, tena mkubwa; lakini watu waliomo walikuwa wachache, na nyumba zilikuwa hazijajengwa. Mungu wangu akanitia moyoni mwangu, kwamba niwakusanye wakuu na maofisa, na watu, ili wahesabiwe kwa nasaba. Nikakiona kitabu cha vizazi vya hao waliokwea hapo kwanza, nikaona ya kwamba imeandikwa humo; Hawa ndio wana wa wilaya, waliokwea kutoka katika ule uhamisho wa hao waliokuwa wamechukuliwa, ambao Nebukadneza, mfalme wa Babeli, aliwachukua mateka, nao wakarudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake; ndio hawa waliokuja pamoja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu, na Baana. Hii ndiyo idadi ya watu wa watu wa Israeli; Wana wa Paroshi, elfu mbili mia moja sabini na wawili. Wana wa Shefatia, mia tatu sabini na wawili. Wana wa Ara mia sita hamsini na wawili. Wana wa Pahath-Moabu, wa wana wa Yeshua na Yoabu, elfu mbili mia nane na kumi na wanane. Wana wa Elamu, elfu moja mia mbili hamsini na wanne. Wana wa Zatu, mia nane arubaini na watano. Wana wa Zakai, mia saba na sitini. Wana wa Binui, mia sita arubaini na wanane. Wana wa Bebai, mia sita ishirini na wanane. Wana wa Azgadi, elfu mbili mia tatu ishirini na wawili. Wana wa Adonikamu, mia sita sitini na saba. Wana wa Bigwai, elfu mbili sitini na saba. Wana wa Adini, mia sita hamsini na watano. Wana wa Ateri, wa Hezekia, tisini na wanane. Wana wa Hashumu, mia tatu ishirini na wanane. Wana wa Besai, mia tatu ishirini na wanne. Wana wa Harifu, mia moja na kumi na wawili. Wana wa Gibeoni, tisini na watano. Watu wa Bethlehemu na Netofa, mia moja na themanini na wanane. Watu wa Anathothi, mia moja ishirini na wanane. Watu wa Beth-Azmawethi, arubaini na wawili. Watu wa Kiriath-Yearimu, na Kefira, na Beerothi, mia saba arubaini na watatu. Watu wa Rama na Geba, mia sita na ishirini na mmoja. Watu wa Mikmashi, mia moja na ishirini na wawili. Watu wa Betheli na Ai, mia moja ishirini na watatu. Watu wa Nebo, hamsini na wawili. Wana wa Elamu wa pili, elfu moja mia mbili hamsini na wanne. Wana wa Harimu, mia tatu na ishirini. Wana wa Yeriko, mia tatu arubaini na watano. Wana wa Lodi, na Hadidi, na Ono, mia saba ishirini na mmoja. Watu wa Senaa, elfu tatu mia tisa na thelathini. Makuhani; Wana wa Yedaya, wa mbari ya Yeshua, mia tisa sabini na watatu. Wana wa Imeri, elfu moja hamsini na wawili. Wana wa Pashuri, elfu moja mia mbili arubaini na saba. Wana wa Harimu, elfu moja na kumi na saba. Walawi; Wana wa Yeshua, wa Kadmieli wa wana wa Hodavia, sabini na wanne. Waimbaji; Wana wa Asafu, mia moja arubaini na wanane. Mabawabu; Wana wa Shalumu, wana wa Ateri, wana wa Talmoni, wana wa Akubu, wana wa Hatita, wana wa Shobai, mia moja thelathini na wanane. Wanethini; wana wa Siha, wana wa Hasufa, wana wa Tabaothi; wana wa Kerosi, wana wa Siaha, wana wa Padoni; wana wa Lebana, wana wa Hagaba, wana wa Salmai; wana wa Hanani, wana wa Gideli, wana wa Gahari; wana wa Reaya, wana wa Resini, wana wa Nekoda; wana wa Gazamu, wana wa Uza, wana wa Pasea; wana wa Besai wana wa Meunimu, wana wa Nefusimu; wana wa Bakbuki, wana wa Hakufa, wana wa Harhuri; wana wa Basluthi, wana wa Mehida, wana wa Harsha; wana wa Barkosi, wana wa Sisera, wana wa Tema; wana wa Nesia, wana wa Hatifa. Wazawa wa watumishi wa Sulemani; Wana wa Sotai, wana wa Soferethi, wana wa Peruda; wana wa Yaala, wana wa Darkoni, wana wa Gideli; wana wa Shefatia, wana wa Hatili, wana wa Pokereth-Sebaimu, wana wa Amoni. Wanethini wote, pamoja na wazawa wa watumishi wa Sulemani, walikuwa mia tatu tisini na wawili. Na hawa ndio watu waliokwea kutoka Tel-mela, na Tel-harsha, na Kerubu, na Adani, na Imeri; lakini hawakuweza kuonesha mbari za baba zao, wala kizazi chao, kwamba walikuwa wa Israeli; Wana wa Delaya, wana wa Tobia, wana wa Nekoda, mia sita na arubaini na wawili. Tena katika makuhani; Wana wa Habaya, wana wa Hakosi, wana wa Barzilai, yule aliyeoa mmojawapo wa binti za Barzilai, Mgileadi, akaitwa kwa jina lao. Hao waliitafuta orodha yao miongoni mwa wale waliohesabiwa kwa nasaba, wasionekane; kwa hiyo walihesabiwa kuwa na unajisi. Na huyo Tirshatha akawaambia kwamba wasile katika vile vitu vitakatifu sana, hata atakaposimama kuhani mwenye Urimu na Thumimu. Basi hilo kusanyiko lote zima, jumla yake ilikuwa watu elfu arubaini na mbili, mia tatu na sitini, tena zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao wanaume kwa wanawake, ambao walikuwa elfu saba na mia tatu na thelathini na saba; kisha walikuwa na waimbaji wanaume kwa wanawake mia mbili arubaini na watano. Farasi wao walikuwa mia saba thelathini na sita; nyumbu zao, mia mbili arubaini na watano; ngamia wao, mia nne thelathini na watano; punda zao, elfu sita na mia saba na ishirini. Na baadhi ya wakuu wa mbari za mababa walitoa mali kwa ajili ya kazi hii. Yule Tirshatha akatoa kwa ajili ya hazina darkoni, za dhahabu elfu moja, na mabeseni hamsini, na mavazi ya makuhani mia tano na thelathini. Na baadhi ya wakuu wa mbari za mababa wakatoa, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni za dhahabu elfu ishirini, na mane za fedha elfu mbili na mia mbili. Na mabaki ya watu wakatoa darkoni za dhahabu elfu ishirini, na mane za fedha elfu mbili, na mavazi ya makuhani sitini na saba.
Nehemia 7:1-72 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ikawa, hapo ukuta ulipojengwa, na milango nimekwisha kuisimamisha, na mabawabu, na waimbaji, na Walawi, wamewekwa, ndipo nilimwagiza ndugu yangu, Hanani, pamoja na yule Hanania, jemadari wa ngome, kuwa na amri juu ya Yerusalemu; kwa maana alikuwa mtu mwaminifu huyo, na mwenye kumcha Mungu kuliko wengi. Nikawaambia, Yasifunguliwe malango ya Yerusalemu kabla halijachomoza jua; nao walinzi wangali wakisimama bado, waifunge milango, mkaikaze; kisha wekeni walinzi wa zamu wa hao wakaao Yerusalemu, kila mtu na zamu yake, na kila mtu kuielekea nyumba yake. Basi mji ulikuwa wa nafasi nyingi, tena mkubwa; lakini watu waliomo walikuwa haba, wala nyumba hazijajengwa. Mungu wangu akanitia moyoni mwangu, kwamba niwakusanye wakuu na mashehe, na watu, ili wahesabiwe kwa nasaba. Nikakiona kitabu cha vizazi vya hao waliokwea hapo kwanza, nikaona ya kwamba imeandikwa humo; Hawa ndio wana wa wilaya, waliokwea kutoka katika ule uhamisho wa hao waliokuwa wamechukuliwa, ambao Nebukadreza, mfalme wa Babeli, aliwachukua mateka, nao wakarudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake; ndio hawa waliokuja pamoja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu, na Baana. Hii ndiyo hesabu ya wanaume wa watu wa Israeli; Wana wa Paroshi, elfu mbili mia moja sabini na wawili. Wana wa Shefatia, mia tatu sabini na wawili. Wana wa Ara mia sita hamsini na wawili. Wana wa Pahath-Moabu, wa wana wa Yeshua na Yoabu, elfu mbili mia nane na kumi na wanane. Wana wa Elamu, elfu moja mia mbili hamsini na wanne. Wana wa Zatu, mia nane arobaini na watano. Wana wa Zakai, mia saba na sitini. Wana wa Binui, mia sita arobaini na wanane. Wana wa Bebai, mia sita ishirini na wanane. Wana wa Azgadi, elfu mbili mia tatu ishirini na wawili. Wana wa Adonikamu, mia sita sitini na saba. Wana wa Bigwai, elfu mbili sitini na saba. Wana wa Adini, mia sita hamsini na watano. Wana wa Ateri, wa Hezekia, tisini na wanane. Wana wa Hashumu, mia tatu ishirini na wanane. Wana wa Besai, mia tatu ishirini na wanne. Wana wa Harifu, mia moja na kumi na wawili. Wana wa Gibeoni, tisini na watano. Watu wa Bethlehemu na Netofa, mia na themanini na wanane. Watu wa Anathothi, mia na ishirini na wanane. Watu wa Beth-Azmawethi, arobaini na wawili. Watu wa Kiriath-Yearimu, na Kefira, na Beerothi, mia saba arobaini na watatu. Watu wa Rama na Geba, mia sita na ishirini na mmoja. Watu wa Mikmashi, mia moja na ishirini na wawili. Watu wa Betheli na Ai, mia moja ishirini na watatu. Watu wa Nebo, hamsini na wawili. Wana wa Elamu wa pili, elfu moja mia mbili hamsini na wanne. Wana wa Harimu, mia tatu na ishirini. Wana wa Yeriko, mia tatu arobaini na watano. Wana wa Lodi, na Hadidi, na Ono, mia saba ishirini na mmoja. Watu wa Senaa, elfu tatu mia kenda na thelathini. Makuhani; Wana wa Yedaya, wa mbari ya Yeshua, mia kenda sabini na watatu. Wana wa Imeri, elfu moja hamsini na wawili. Wana wa Pashuri, elfu moja mia mbili arobaini na saba. Wana wa Harimu, elfu moja na kumi na saba. Walawi; Wana wa Yeshua, wa Kadmieli wa wana wa Hodavia, sabini na wanne. Waimbaji; Wana wa Asafu, mia moja arobaini na wanane. Mabawabu; Wana wa Shalumu, wana wa Ateri, wana wa Talmoni, wana wa Akubu, wana wa Hatita, wana wa Shobai, mia moja thelathini na wanane. Wanethini; wana wa Siha, wana wa Hasufa, wana wa Tabaothi; wana wa Kerosi, wana wa Siaha, wana wa Padoni; wana wa Lebana, wana wa Hagaba, wana wa Salmai; wana wa Hanani, wana wa Gideli, wana wa Gahari; wana wa Reaya, wana wa Resini, wana wa Nekoda; wana wa Gazamu, wana wa Uza, wana wa Pasea; wana wa Besai wana wa Meunimu, wana wa Nefusimu; wana wa Bakbuki, wana wa Hakufa, wana wa Harhuri; wana wa Basluthi, wana wa Mehida, wana wa Harsha; wana wa Barkosi, wana wa Sisera, wana wa Tema; wana wa Nesia, wana wa Hatifa. Akina watumwa wa Sulemani; Wana wa Sotai, wana wa Soferethi, wana wa Peruda; wana wa Yaala, wana wa Darkoni, wana wa Gideli; wana wa Shefatia, wana wa Hatili, wana wa Pokereth-Sebaimu, wana wa Amoni. Wanethini wote, pamoja na akina watumwa wa Sulemani, walikuwa mia tatu tisini na wawili. Na hawa ndio watu waliokwea kutoka Tel-mela, na Tel-harsha, na Kerubu, na Adani, na Imeri; walakini hawakuweza kuonyesha mbari za baba zao, wala kizazi chao, kwamba walikuwa wa Israeli; Wana wa Delaya, wana wa Tobia, wana wa Nekoda, mia sita na arobaini na wawili. Tena katika makuhani; Wana wa Habaya, wana wa Hakosi, wana wa Barzilai, yule aliyeoa mmojawapo binti Barzilai, Mgileadi, akaitwa kwa jina lao. Hao waliitafuta orodha yao miongoni mwa wale waliohesabiwa kwa nasaba, wasionekane; kwa hiyo walihesabiwa kuwa na unajisi. Na huyo Tirshatha akawaambia kwamba wasile katika vile vitu vitakatifu sana, hata atakaposimama kuhani mwenye Urimu na Thumimu. Basi hilo kusanyiko lote zima, jumla yake ilikuwa watu arobaini na mbili elfu na mia tatu na sitini, tena zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao waume kwa wake, ambao walikuwa elfu saba na mia tatu na thelathini na saba; kisha walikuwa na waimbaji waume kwa wake mia mbili arobaini na watano. Farasi zao walikuwa mia saba thelathini na sita; nyumbu zao, mia mbili arobaini na watano; ngamia zao, mia nne thelathini na watano; punda zao, elfu sita na mia saba na ishirini. Na baadhi ya wakuu wa mbari za mababa walitoa mali kwa ajili ya kazi hii. Yule Tirshatha akatoa kwa ajili ya hazina darkoni za dhahabu elfu moja, na mabakuli hamsini, na mavazi ya makuhani mia tano na thelathini. Na baadhi ya wakuu wa mbari za mababa wakatoa, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni za dhahabu ishirini elfu, na mane za fedha elfu mbili na mia mbili. Na mabaki ya watu wakatoa darkoni za dhahabu ishirini elfu, na mane za fedha elfu mbili, na mavazi ya makuhani sitini na saba.
Nehemia 7:1-72 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Baada ya ukuta kukamilika kujengwa upya na nikaweka milango, mabawabu wa lango, waimbaji, na Walawi waliteuliwa. Nikamweka Hanani ndugu yangu kuwa kiongozi wa Yerusalemu, pamoja na Hanania jemadari wa ngome, kwa kuwa alikuwa mtu mwadilifu na mwenye kumcha Mungu kuliko watu wengine. Nikawaambia, “Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe hadi jua litakapokuwa limepanda. Walinzi wa malango wakiwa bado kwenye zamu, waamuru wafunge milango na waweke makomeo. Pia wateueni wenyeji wa Yerusalemu wawe walinzi, kila mmoja kwenye lindo lake, na wengine karibu na nyumba zao wenyewe.” Mji ulikuwa mkubwa, tena wenye nafasi nyingi, lakini walikuwepo watu wachache ndani yake, nazo nyumba zilikuwa bado ni magofu. Hivyo Mungu wangu akaweka moyoni mwangu kuwakusanya wakuu, maafisa na watu kwa ajili ya kuorodheshwa kulingana na jamaa zao. Nilikuta orodha ya vizazi ya wale waliokuwa wa kwanza kurudi toka utumwani. Haya ndio niliyokuta yameandikwa humo: Hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Azaria, Raamia, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispereti, Bigwai, Nehumu na Baana): Orodha ya wanaume wa Israeli ilikuwa: wazao wa Paroshi, elfu mbili mia moja sabini na wawili (2,172); wazao wa Shefatia, mia tatu sabini na wawili (372); wazao wa Ara, mia sita hamsini na wawili (652); wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu), elfu mbili mia nane na kumi na nane (2,818); wazao wa Elamu, elfu moja mia mbili hamsini na wanne (1,254); wazao wa Zatu, mia nane arobaini na watano (845); wazao wa Zakai, mia saba na sitini (760); wazao wa Binui, mia sita ishirini na wanne (648); wazao wa Bebai, mia sita ishirini na nane (628); wazao wa Azgadi, elfu mbili mia tatu ishirini na wawili (2,322); wazao wa Adonikamu, mia sita sitini na saba (667); wazao wa Bigwai, elfu mbili na sitini na saba (2,067); wazao wa Adini, mia sita hamsini na watano (655); wazao wa Ateri (kupitia Hezekia), tisini na nane (98); wazao wa Hashumu, mia tatu ishirini na nane (328); wazao wa Besai, mia tatu ishirini na wanne (324); wazao wa Harifu, mia moja na kumi na wawili (112); wazao wa Gibeoni, tisini na watano (95); watu wa Bethlehemu na Netofa, mia moja na themanini na nane (188); watu wa Anathothi, mia moja ishirini na nane (128); watu wa Beth-Azmawethi, arobaini na wawili (42); watu wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi, mia saba arobaini na watatu (743); watu wa Rama na Geba, mia sita ishirini na mmoja (621); watu wa Mikmashi, mia moja ishirini na wawili (122); watu wa Betheli na Ai, mia moja ishirini na watatu (123); watu wa Nebo, hamsini na wawili (52); wazao wa Elamu, elfu moja mia mbili hamsini na wanne (1,254); wazao wa Harimu, mia tatu na ishirini (320); wazao wa Yeriko, mia tatu arobaini na watano (345); wazao wa Lodi, Hadidi na Ono, mia saba ishirini na mmoja (721); wazao wa Senaa, elfu tatu mia tisa na thelathini (3,930). Makuhani: wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua), mia tisa sabini na watatu (973); wazao wa Imeri, elfu moja hamsini na wawili (1,052); wazao wa Pashuri, elfu moja mia mbili arobaini na saba (1,247); wazao wa Harimu, elfu moja na kumi na saba (1,017). Walawi: wazao wa Yeshua (kupitia Kadmieli kupitia jamaa ya Hodavia), sabini na wanne (74). Waimbaji: wazao wa Asafu, mia moja arobaini na nane (148). Mabawabu wa malango: wazao wa Shalumu, Ateri, Talmoni, Akubu, Hatita na Shobai, mia moja thelathini na nane (138). Watumishi wa Hekalu: wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi, wazao wa Kerosi, Sia, Padoni, wazao wa Lebana, Hagaba, Shalmai, wazao wa Hanani, Gideli, Gahari, wazao wa Reaya, Resini, Nekoda, wazao wa Gazamu, Uza, Pasea, wazao wa Besai, Meunimu, Nefusimu, wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri, wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha, wazao wa Barkosi, Sisera, Tema, wazao wa Nesia na Hatifa. Wazao wa watumishi wa Sulemani: wazao wa Sotai, Soferethi, Perida, Yaala, Darkoni, Gideli, Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Amoni. Watumishi wa Hekalu, na wazao wa watumishi wa Sulemani, mia tatu tisini na wawili (392). Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli: wazao wa Delaya, Tobia na Nekoda, mia sita arobaini na wawili (642). Kutoka miongoni mwa makuhani: wazao wa Hobaya, wa Hakosi na wa Barzilai (mtu aliyemwoa binti Barzilai Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo). Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa ukuhani, kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. Kwa hiyo, mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu. Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa elfu arobaini na mbili, mia tatu na sitini (42,360); tena zaidi ya hao walikuwa na watumishi wa kiume na wa kike elfu saba, mia tatu na thelathini na saba (7,337); pia walikuwa na waimbaji wanaume na wanawake mia mbili arobaini na watano (245). Walikuwa na farasi mia saba thelathini na sita (736), nyumbu mia mbili arobaini na watano (245), ngamia mia nne thelathini na watano (435) na punda elfu sita, mia saba na ishirini (6,720). Baadhi ya viongozi wa jamaa walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala alikabidhi kwenye hazina darkoni elfu moja za dhahabu, mabakuli hamsini, na mavazi mia tano na thelathini ya makuhani. Baadhi ya viongozi wa jamaa walikabidhi kwenye hazina darkoni elfu ishirini za dhahabu, na mane elfu mbili na mia mbili za fedha kwa ajili ya kazi hiyo. Jumla ya matoleo ya watu wengine yalikuwa ni darkoni elfu ishirini za dhahabu, mane elfu mbili za fedha, na mavazi sitini na saba ya makuhani.