Nehemia 1:7-9
Nehemia 1:7-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Tumetenda mabaya mbele yako, hatujazishika amri zako, kanuni na maagizo yako uliyomwagiza mtumishi wako Mose. Kumbuka sasa lile ulilomwambia mtumishi wako Mose, uliposema, ‘Kama hamtakuwa waaminifu, nitawatawanya miongoni mwa mataifa. Lakini mkinirudia, mkazishika amri zangu na kuzifuata hata ingawa nitakuwa nimewatawanya mbali kabisa, nitawarudisha mahali nilipochagua kuwa mahali pangu pa kuabudiwa.’
Nehemia 1:7-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tumetenda maovu mengi juu yako, wala hatukuzishika amri, wala sheria, wala hukumu, ulizomwamuru Musa, mtumishi wako. Nakuomba, likumbuke neno lile ulilomwamuru Musa, mtumishi wako, ukisema, Mkikosa, nitawatawanya kati ya mataifa; bali mkinirudia mimi, na kuzishika amri zangu na kuzitenda, watu wako waliofukuzwa wajapokuwa katika pande za mwisho za mbingu, hata hivyo nitawakusanya kutoka huko, na kuwaleta mpaka mahali pale nilipopachagua ili kuliweka jina langu hapo.
Nehemia 1:7-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tumetenda maovu mengi juu yako, wala hatukuzishika amri, wala sheria, wala hukumu, ulizomwamuru Musa, mtumishi wako. Nakuomba, likumbuke neno lile ulilomwamuru Musa, mtumishi wako, ukisema, Mkikosa, nitawatawanya kati ya mataifa; bali mkinirudia mimi, na kuzishika amri zangu na kuzitenda, watu wako waliofukuzwa wajapokuwa katika pande za mwisho za mbingu, hata hivyo nitawakusanya kutoka huko, na kuwaleta mpaka mahali pale nilipopachagua ili kuliweka jina langu hapo.
Nehemia 1:7-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Tumetenda uovu sana mbele zako. Hatukutii amri, maagizo na sheria ulizompa Musa mtumishi wako. “Kumbuka agizo ulilompa Musa mtumishi wako, ukisema, ‘Mkikosa uaminifu, nitawatawanya miongoni mwa mataifa, lakini mkinirudia na kutii amri zangu, ndipo hata kama watu wenu walio uhamishoni katika miisho ya dunia, nitawakusanya kutoka huko na kuwaleta mahali nilipopachagua kuwa makao kwa ajili ya Jina langu.’