Nehemia 1:3-4
Nehemia 1:3-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Wao wakaniambia, “Wayahudi waliosalimika na kubaki katika mkoa ule, wako katika taabu na aibu. Ukuta wa mji wa Yerusalemu umebomolewa na malango yake yameteketea.” Niliposikia hayo nilikaa chini na kulia, nikaomboleza kwa siku kadhaa. Nikafunga na kumwomba Mungu wa mbinguni
Nehemia 1:3-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wakaniambia, Watu waliosalimika, waliosalia huko katika mkoa ule, wamo katika hali ya dhiki kubwa na aibu; tena ukuta wa Yerusalemu umebomolewa, na malango yake yameteketezwa kwa moto. Hapo niliposikia maneno hayo, nikaketi, nikalia, nikaomboleza siku kadhaa; kisha nikafunga, nikaomba mbele za Mungu wa mbinguni
Nehemia 1:3-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wakaniambia, Watu wa uhamisho, waliosalia huko katika wilaya ile, wamo katika hali ya dhiki nyingi na mashutumu; tena ukuta wa Yerusalemu umebomolewa, na malango yake yameteketezwa kwa moto. Hata ikawa niliposikia maneno hayo, nikaketi, nikalia, nikaomboleza siku kadha wa kadha; kisha nikafunga, nikaomba mbele za Mungu wa mbinguni
Nehemia 1:3-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Wakaniambia, “Wale walionusurika kwenda uhamishoni, wale ambao wamerudi kwenye lile jimbo, wako katika taabu kubwa na aibu. Ukuta wa Yerusalemu umebomoka, na malango yake yamechomwa moto.” Niliposikia mambo haya, niliketi, nikalia. Kwa siku kadhaa niliomboleza na kufunga na kuomba mbele za Mungu wa mbinguni.