Nehemia 1:1-2
Nehemia 1:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Lifuatalo ni simulizi la Nehemia, mwana wa Hakalia. Ikawa, nilipokuwa katika mji mkuu wa Susa, katika mwezi wa Kislevu wa mwaka wa ishirini, Hanani, mmoja wa ndugu zangu, akaja pamoja na baadhi ya watu toka nchini Yuda. Nikawauliza kuhusu Wayahudi wenzetu waliosalimika, yaani ambao hawakuhamishiwa Babuloni na kuhusu mji wa Yerusalemu.
Nehemia 1:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Habari za Nehemia, mwana wa Hakalia. Ikawa katika mwezi wa Kislevu, mwaka wa ishirini, nilipokuwapo Shushani ngomeni, Hanani, mmoja wa ndugu zangu, akanijia, yeye na watu wengine waliotoka Yuda; nami nikawauliza habari za Wayahudi waliosalimika, ambao hawakuchukuliwa uhamishoni na habari za Yerusalemu.
Nehemia 1:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Habari za Nehemia, mwana wa Hakalia. Ikawa katika mwezi wa Kisleu, mwaka wa ishirini, nilipokuwapo Shushani ngomeni, Hanani, mmoja wa ndugu zangu, akanijia, yeye na watu wengine waliotoka Yuda; nami nikawauliza habari za Wayahudi waliopona, hao watu wa uhamisho waliosalia; na habari za Yerusalemu.
Nehemia 1:1-2 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Maneno ya Nehemia mwana wa Hakalia: Katika mwezi wa Kislevu katika mwaka wa ishirini, wakati nilikuwa ngomeni katika jumba la kifalme la Shushani, Hanani, mmoja wa ndugu zangu, alikuja kutoka Yuda akiwa na watu wengine, nami nikawauliza kuhusu mabaki ya Wayahudi wale walionusurika kwenda uhamishoni na pia kuhusu Yerusalemu.