Nahumu 1:2-3
Nahumu 1:2-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu ni Mungu mwenye wivu, mlipiza kisasi; Mwenyezi-Mungu hulipiza kisasi na ni mwenye ghadhabu; Mwenyezi-Mungu hulipiza kisasi kwa adui zake, huwaka ghadhabu juu ya adui zake. Mwenyezi-Mungu hakasiriki upesi, lakini amejaa nguvu, Mwenyezi-Mungu kamwe hatawaachilia wenye hatia. Apitapo Mwenyezi-Mungu, huzuka kimbunga na dhoruba; mawingu ni vumbi litimuliwalo na nyayo zake.
Nahumu 1:2-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA ni Mungu mwenye wivu, naye hujilipiza kisasi; BWANA hujilipiza kisasi, naye ni mwingi wa hasira; BWANA hujilipiza kisasi juu ya adui zake, huwawekea adui zake akiba ya hasira. BWANA si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; BWANA ana njia yake katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake.
Nahumu 1:2-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA ni Mungu mwenye wivu, naye hujilipiza kisasi; BWANA hujilipiza kisasi, naye ni mwingi wa hasira; BWANA hujilipiza kisasi juu ya adui zake, huwawekea adui zake akiba ya hasira. BWANA si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; BWANA ana njia yake katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake.
Nahumu 1:2-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
BWANA ni mwenye wivu na Mungu mlipiza kisasi; BWANA hulipiza kisasi na amejaa ghadhabu. BWANA hulipiza kisasi juu ya watesi wake, naye anadumisha ghadhabu yake dhidi ya adui zake. BWANA si mwepesi wa hasira naye ni mwenye nguvu, BWANA hataacha kuadhibu wenye hatia. Njia yake ipo katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni vumbi la miguu yake.