Marko 6:5-6 - Compare All Versions
Marko 6:5-6 BHN (Biblia Habari Njema)
Hakuweza kutenda miujiza hapo, ila aliwawekea mikono wagonjwa wachache, akawaponya. Alishangaa sana kwa sababu ya kutoamini kwao. Kisha Yesu alivitembelea vijiji vya pale karibu akiwafundisha watu.
Marko 6:5-6 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Wala hakuweza kufanya mwujiza wowote huko, isipokuwa aliweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache, akawaponya. Akastaajabu kwa sababu ya kutoamini kwao. Akazungukazunguka katika vile vijiji, akifundisha.
Marko 6:5-6 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala hakuweza kufanya mwujiza wo wote huko, isipokuwa aliweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache, akawaponya. Akastaajabu kwa sababu ya kutokuamini kwao. Akazunguka-zunguka katika vile vijiji, akifundisha.
Marko 6:5-6 NEN (Neno)
Hakufanya miujiza yoyote huko isipokuwa kuweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache na kuwaponya. Naye akashangazwa sana kwa kutoamini kwao. Kisha Yesu akawa anaenda kutoka kijiji kimoja hadi kingine akifundisha.