Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mika 3:1-12

Mika 3:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)

Sasa sikilizeni enyi wakuu wa wazawa wa Yakobo, sikilizeni, enyi watawala wa wazawa wa Israeli! Nyinyi ndio mnaopaswa kujua mambo ya haki. Lakini nyinyi mnachukia mema na kupenda maovu. Mnawachuna ngozi watu wangu, na kubambua nyama mifupani mwao. Mnajilisha kwa nyama ya watu wangu mnawachuna ngozi yao, mnaivunjavunja mifupa yao, na kuwakatakata kama nyama ya kupika, kama nyama ya kutia ndani ya chungu. Wakati unakuja ambapo mtamlilia Mwenyezi-Mungu, lakini yeye hatawajibu. Atauficha uso wake wakati huo, kwa sababu mmetenda mambo maovu. Mwenyezi-Mungu asema hivi kuhusu manabii wanaowapotosha watu wake; manabii ambao hutabiri amani wakipewa kitu, lakini huwatishia watu kwa vita wasipopewa kitu: “Kwenu manabii kutakuwa usiku bila maono, kutakuwa giza kwenu bila ufunuo. Kwenu manabii kutakuchwa, mchana utakuwa giza kwenu.” Mabingwa wa maono watafedheheka, mafundi wa kubashiri wataaibishwa; wote watafunga midomo yao, maana hawatapata jibu lolote kutoka kwa Mungu. Lakini kwa upande wangu, nimejazwa nguvu na roho ya Mwenyezi-Mungu; nimejaliwa kujua haki na kuwa na uwezo niwatangazie wazawa wa Yakobo kosa lao, niwaambie Waisraeli dhambi yao. Sikieni jambo hili enyi viongozi wa wazawa wa Yakobo, sikilizeni, enyi watawala wa Waisraeli: Nyinyi mnachukia mambo ya haki na kupotosha mambo ya adili. Nyinyi mnajenga mji wa Siyoni kwa damu, naam, mji wa Yerusalemu kwa dhuluma. Waamuzi hufanya kazi yao kwa rushwa, makuhani wake hufundisha kwa malipo, manabii hutabiri kwa fedha. Hata hivyo hujidai kumtegemea Mwenyezi-Mungu, wakisema, “Mwenyezi-Mungu, si yupo pamoja nasi? Hatutapatwa na madhara yoyote!” Haya! Kwa sababu yenu, Siyoni utalimwa kama shamba, Yerusalemu utakuwa magofu, nao mlima wa hekalu utakuwa msitu.

Shirikisha
Soma Mika 3

Mika 3:1-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Nikasema, Tafadhali sikieni, enyi vichwa vya Yakobo, mnaoitawala nyumba ya Israeli. Je! Haiwapasi ninyi kujua hukumu? Ninyi mnaoyachukia mema, na kuyapenda mabaya; ninyi mnaowachuna watu ngozi yao, na nyama mifupani mwao. Naam, mnakula nyama ya watu wangu, na kuwachuna ngozi zao, na kuivunja mifupa yao; naam, kuwakata vipande vipande kama kwa kutiwa chunguni, na kama nyama sufuriani. Ndipo watakapomwomba BWANA, asiwaitikie; naam, atawaficha uso wake wakati huo, kwa kadiri walivyotenda mabaya kwa matendo yao. BWANA asema hivi kuhusu manabii wanaowakosesha watu wangu; hao waumao kwa meno yao, na kulia, Amani; na mtu awaye yote asiyetia kitu vinywani mwao, wao humwandalia vita. Kwa hiyo itakuwa usiku kwenu, msipate kuona maono; tena itakuwa giza kwenu, msiweze kubashiri; nalo jua litawachwea manabii, nao mchana utakuwa mweusi juu yao. Na hao waonaji wataaibika, na wenye kubashiri watafadhaika; naam, hao wote watajifunika midomo yao; kwa maana; hapana jawabu la Mungu. Bali mimi, hakika nimejaa nguvu kwa Roho ya BWANA; nimejaa hukumu na uwezo; nimhubirie Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake. Sikieni haya, tafadhali, enyi vichwa vya nyumba ya Yakobo, mnaoitawala nyumba ya Israeli, mnaochukia hukumu, na kuipotosha adili. Wanaoijenga Sayuni kwa damu, na Yerusalemu kwa uovu. Wakuu wake huhukumu ili wapate rushwa, na makuhani wake hufundisha ili wapate ijara, na manabii wake hubashiri ili wapate fedha; ila hata hivyo watamtegemea BWANA, na kusema, Je! Hayupo BWANA katikati yetu? Hapana neno baya lolote litakalotufikia. Basi, kwa ajili yenu, Sayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu; na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni.

Shirikisha
Soma Mika 3

Mika 3:1-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Nikasema, Tafadhali sikieni, enyi vichwa vya Yakobo, mnaoitawala nyumba ya Israeli. Je! Haiwapasi ninyi kujua hukumu? Ninyi mnaoyachukia mema, na kuyapenda mabaya; ninyi mnaowachuna watu ngozi yao, na nyama mifupani mwao. Naam, mnakula nyama ya watu wangu, na kuwachuna ngozi zao, na kuivunja mifupa yao; naam, kuwakata vipande vipande kama kwa kutiwa chunguni, na kama nyama sufuriani. Ndipo watakapomwomba BWANA, asiwaitikie; naam, atawaficha uso wake wakati huo, kwa kadiri walivyotenda mabaya kwa matendo yao. BWANA asema hivi katika habari za manabii wanaowakosesha watu wangu; hao waumao kwa meno yao, na kulia, Amani; na mtu awaye yote asiyetia kitu vinywani mwao, wao humwandalia vita. Kwa hiyo itakuwa usiku kwenu, msipate kuona maono; tena itakuwa giza kwenu, msiweze kubashiri; nalo jua litawachwea manabii, nao mchana utakuwa mweusi juu yao. Na hao waonaji watatahayarika, na wenye kubashiri watafadhaika; naam, hao wote watajifunika midomo yao; kwa maana; hapana jawabu la Mungu. Bali mimi, hakika nimejaa nguvu kwa roho ya BWANA; nimejaa hukumu na uwezo; nimhubiri Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake. Sikieni haya, tafadhali, enyi vichwa vya nyumba ya Yakobo, mnaoitawala nyumba ya Israeli, mnaochukia hukumu, na kuipotosha adili. Wanaijenga Sayuni kwa damu, na Yerusalemu kwa uovu. Wakuu wake huhukumu ili wapate rushwa, na makuhani wake hufundisha ili wapate ijara, na manabii wake hubashiri ili wapate fedha; ila hata hivyo watamtegemea BWANA, na kusema, Je! Hayupo BWANA katikati yetu? Hapana neno baya lo lote litakalotufikia. Basi, kwa ajili yenu, Sayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu; na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni.

Shirikisha
Soma Mika 3

Mika 3:1-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Kisha nikasema, “Sikilizeni enyi viongozi wa Yakobo, enyi watawala wa nyumba ya Israeli. Je, hampaswi kujua hukumu, ninyi mnaochukia mema na kupenda maovu; ninyi mnaowachuna watu wangu ngozi na kuondoa nyama kwenye mifupa yao; ninyi mnaokula nyama ya watu wangu, mnaowachuna ngozi na kuvunja mifupa yao vipande vipande; mnaowakatakata kama nyama ya kuwekwa kwenye sufuria na kama nyama ya kuwekwa kwenye chungu?” Kisha watamlilia BWANA, lakini hatawajibu. Wakati huo atawaficha uso wake kwa sababu ya uovu waliotenda. Hili ndilo asemalo BWANA: “Kuhusu manabii wanaowapotosha watu wangu, mtu akiwalisha, wanatangaza ‘amani’; kama hakufanya hivyo, wanaandaa kupigana vita dhidi yake. Kwa hiyo usiku utawajieni, msiweze kuwa na maono, na giza, msiweze kubashiri. Jua litawachwea manabii hao, nao mchana utakuwa giza kwao. Waonaji wataaibika na waaguzi watafedheheka. Wote watafunika nyuso zao kwa sababu hakuna jibu litokalo kwa Mungu.” Lakini mimi nimejazwa nguvu, nimejazwa Roho wa BWANA, haki na uweza, kumtangazia Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake. Sikieni hili, enyi viongozi wa nyumba ya Yakobo, enyi watawala wa nyumba ya Israeli, mnaodharau haki na kupotosha kila lililo sawa; mnaojenga Sayuni kwa kumwaga damu na Yerusalemu kwa uovu. Viongozi wake wanahukumu kwa rushwa, na makuhani wake wanafundisha kwa malipo, nao manabii wake wanatabiri kwa fedha. Hata hivyo wanamwegemea BWANA na kusema, “Je, BWANA si yumo miongoni mwetu? Hakuna maafa yatakayotupata.” Kwa ajili yenu, Sayuni italimwa kama shamba, Yerusalemu itakuwa lundo la kokoto, na kilima cha Hekalu kitakuwa kichuguu kilichofunikwa na vichaka.

Shirikisha
Soma Mika 3