Mika 1:2-4
Mika 1:2-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Sikilizeni enyi watu wote; sikiliza ewe dunia na vyote vilivyomo. Mwenyezi-Mungu anakuja kuwashtaki, Bwana anena kutoka hekalu lake takatifu. Naam! Mwenyezi-Mungu yuaja kutoka makao yake; atashuka na kutembea juu ya vilele vya dunia. Milima itayeyuka chini ya nyayo zake, kama nta karibu na moto; mabonde yatapasuka, kama maji yaporomokayo kwenye mteremko.
Mika 1:2-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Sikilizeni, enyi watu wa kabila zote; sikiliza, Ee dunia, na vyote vilivyomo; Bwana MUNGU na ashuhudie juu yenu, yeye Bwana kutoka hekalu lake takatifu. Kwa maana, angalieni, BWANA anakuja akitoka mahali pake, naye atashuka, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka. Na hiyo milima itayeyuka chini yake, nayo mabonde yatapasuliwa, kama vile nta iliyo mbele ya moto, kama maji yaliyomwagika katika mteremko.
Mika 1:2-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Sikilizeni, enyi watu wa kabila zote; sikiliza, Ee dunia, na vyote vilivyomo; Bwana MUNGU na ashuhudie juu yenu, yeye Bwana kutoka hekalu lake takatifu. Kwa maana, angalieni, BWANA anakuja akitoka mahali pake, naye atashuka, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka. Na hiyo milima itayeyuka chini yake, nayo mabonde yatapasuliwa, kama vile nta iliyo mbele ya moto, kama maji yaliyomwagika tena kutelemka gengeni.
Mika 1:2-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Sikieni, enyi mataifa, enyi nyote, sikilizeni, ee dunia na wote mliomo, ili BWANA Mwenyezi ashuhudie dhidi yenu, Bwana kutoka Hekalu lake takatifu. Tazama! BWANA anakuja kutoka mahali pake; anashuka na kukanyaga mahali palipoinuka juu pa dunia. Milima inayeyuka chini yake na mabonde yanagawanyika kama nta mbele ya moto, kama maji yanayotiririka kasi kwenye mteremko.