Mathayo 7:9-11
Mathayo 7:9-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Je, kuna yeyote miongoni mwenu ambaye mtoto wake akimwomba mkate, atampa jiwe? Au je, akimwomba samaki, atampa nyoka? Kama basi nyinyi, ingawa ni waovu, mwajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, hakika Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi: Atawapa mema wale wanaomwomba.
Mathayo 7:9-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? Au akiomba samaki, atampa nyoka? Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu zawadi njema, je! Si Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema zaidi wao wamwombao?
Mathayo 7:9-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? Au akiomba samaki, atampa nyoka? Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?
Mathayo 7:9-11 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Au ni nani miongoni mwenu ambaye mwanawe akimwomba mkate atampa jiwe? Au mwanawe akimwomba samaki atampa nyoka? Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao?