Mathayo 6:10-13
Mathayo 6:10-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo chakula chetu cha kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea. Usitutie katika majaribu, lakini utuokoe na yule Mwovu.’ [ Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]
Mathayo 6:10-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]
Mathayo 6:10-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]
Mathayo 6:10-13 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ufalme wako uje. Mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni. Utupatie riziki yetu ya kila siku. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tulivyokwisha kuwasamehe wadeni wetu. Usitutie majaribuni, bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu [kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amen].’