Mathayo 4:8-11
Mathayo 4:8-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonesha falme zote za ulimwengu na fahari zake, akamwambia, “Hivi vyote nitakupa kama ukipiga magoti na kuniabudu.” Hapo, Yesu akamwambia, “Nenda zako Shetani! Imeandikwa: ‘Utamwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia yeye peke yake.’” Basi, Ibilisi akamwacha, na malaika wakaja, wakamhudumia.
Mathayo 4:8-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka katika mlima mrefu mno, akamwonesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia, Haya yote nitakupa, ukiinama na kunisujudia. Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Mwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake. Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.
Mathayo 4:8-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia. Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.
Mathayo 4:8-11 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kwa mara nyingine, ibilisi akampeleka Yesu hadi kwenye kilele cha mlima mrefu na kumwonesha falme zote za dunia na fahari zake, kisha akamwambia, “Nitakupa hivi vyote ukinisujudia na kuniabudu.” Yesu akamwambia, “Ondoka mbele yangu, Shetani! Kwa maana imeandikwa, ‘Mwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.’” Ndipo ibilisi akamwacha, nao malaika wakaja na kumhudumia.