Mathayo 4:6-7
Mathayo 4:6-7 Biblia Habari Njema (BHN)
akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana imeandikwa: ‘Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako; watakuchukua mikononi mwao, usije ukajikwaa kwenye jiwe.’” Yesu akamwambia, “Imeandikwa pia: ‘Usimjaribu Bwana, Mungu wako.’”
Mathayo 4:6-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.
Mathayo 4:6-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.
Mathayo 4:6-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
akamwambia, “Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini. Kwa kuwa imeandikwa: “ ‘Atakuagizia malaika wake, nao watakuchukua mikononi mwao ili usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.’” Yesu akamjibu, “Pia imeandikwa: ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’”