Mathayo 4:5-6
Mathayo 4:5-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, mji mtakatifu, akamweka juu ya mnara wa hekalu, akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana imeandikwa: ‘Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako; watakuchukua mikononi mwao, usije ukajikwaa kwenye jiwe.’”
Mathayo 4:5-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
Mathayo 4:5-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
Mathayo 4:5-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ndipo ibilisi akampeleka Yesu hadi mji mtakatifu na kumweka juu ya mnara mrefu wa Hekalu, akamwambia, “Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini. Kwa kuwa imeandikwa: “ ‘Atakuagizia malaika wake, nao watakuchukua mikononi mwao ili usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.’”