Mathayo 4:18-20
Mathayo 4:18-20 Biblia Habari Njema (BHN)
Yesu alipokuwa anatembea kando ya ziwa Galilaya, aliwaona ndugu wawili wavuvi; Simoni (aitwaye Petro) na Andrea, ndugu yake; walikuwa wakivua samaki kwa nyavu ziwani. Basi, akawaambia, “Nifuateni, nami nitawafanya nyinyi wavuvi wa watu.” Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.
Mathayo 4:18-20 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Naye alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi. Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.
Mathayo 4:18-20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Naye alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi. Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.
Mathayo 4:18-20 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Yesu alipokuwa akitembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea ndugu yake. Walikuwa wakizitupa nyavu zao baharini kwa kuwa walikuwa wavuvi. Yesu akawaambia, “Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu.” Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.