Mathayo 4:12-16
Mathayo 4:12-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Yesu aliposikia kwamba Yohane ametiwa gerezani alikwenda Galilaya. Aliondoka Nazareti, akaenda Kafarnaumu, mji ulio kando ya bahari ya Genesareti, mpakani mwa wilaya za Zebuluni na Naftali, akakaa huko. Ndivyo lilivyotimia lile neno lililosemwa kwa njia ya nabii Isaya: “Nchi ya Zebuluni na nchi ya Naftali, kuelekea baharini ngambo ya mto Yordani, Galilaya, nchi ya watu wa mataifa! Watu waliokaa gizani wameona mwanga mkubwa. Nao walioishi katika nchi ya giza na kivuli cha kifo, mwanga umewaangazia!”
Mathayo 4:12-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya; akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali; ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, Njia ya bahari, ng'ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa, Watu wale waliokaa katika giza Wameona mwanga mkuu, Nao waliokaa katika nchi na uvuli wa mauti Mwanga umewazukia.
Mathayo 4:12-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya; akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali; ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, Njia ya bahari, ng’ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa, Watu wale waliokaa katika giza Wameona mwanga mkuu, Nao waliokaa katika nchi na uvuli wa mauti Mwanga umewazukia.
Mathayo 4:12-16 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Yesu aliposikia kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa amefungwa gerezani, alirudi Galilaya. Akaondoka Nazareti akaenda kuishi Kapernaumu, mji ulio karibu na bahari, katika nchi ya Zabuloni na Naftali, ili kutimiza neno lililonenwa na nabii Isaya, aliposema: “Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, kwenye njia ya bahari, ngʼambo ya Yordani, Galilaya ya Mataifa: watu wale waliokaa gizani wameona nuru kuu; nao wale walioishi katika nchi ya uvuli wa mauti, nuru imewazukia.”