Mathayo 23:24-26
Mathayo 23:24-26 Biblia Habari Njema (BHN)
Viongozi vipofu! Mnatoa nzi katika kinywaji, lakini mnameza ngamia! “Ole wenu waalimu wa sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafisha kikombe na bakuli kwa nje, lakini ndani mnaacha kumejaa vitu mlivyopata kwa unyanganyi na uchoyo. Mfarisayo kipofu! Kisafishe kikombe ndani kwanza na nje kutakuwa safi pia.
Mathayo 23:24-26 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia. Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang'anyi na kutokuwa na kiasi. Ewe Farisayo kipofu, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nako kupate kuwa safi.
Mathayo 23:24-26 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia. Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang’anyi na kutokuwa na kiasi. Ewe Farisayo kipofu, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi.
Mathayo 23:24-26 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ninyi viongozi vipofu, mnachuja kiroboto lakini mnameza ngamia! “Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Kwa maana mnasafisha kikombe na sahani kwa nje, lakini ndani mmejaa unyangʼanyi na kutokuwa na kiasi. Ewe Farisayo kipofu! Safisha ndani ya kikombe na sahani kwanza, ndipo nje itakuwa safi pia.