Mathayo 23:1-3
Mathayo 23:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha Yesu akauambia umati wa watu pamoja na wanafunzi wake, “Waalimu wa sheria na Mafarisayo wana mamlaka ya kufafanua sheria ya Mose. Kwa hiyo shikeni na kutekeleza chochote watakachowaambieni. Lakini msiyaige matendo yao, maana hawatekelezi yale wanayoyahubiri.
Mathayo 23:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha Yesu akawaambia makutano na wanafunzi wake, akasema, Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa; basi, yoyote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi.
Mathayo 23:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha Yesu akawaambia makutano na wanafunzi wake, akasema, Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa; basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi.
Mathayo 23:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kisha Yesu akaambia wale umati wa watu na wanafunzi wake: “Walimu wa sheria na Mafarisayo wameketi kwenye kiti cha Musa, hivyo inawapasa kuwatii na kufanya kila kitu wanachowaambia. Lakini msifuate yale wanayotenda, kwa sababu hawatendi yale wanayohubiri.