Mathayo 2:3-4 - Linganisha Matoleo Yote
Mathayo 2:3-4 BHN (Biblia Habari Njema)
Mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, yeye pamoja na wakazi wote wa Yerusalemu. Basi, akawaita pamoja makuhani wakuu wote na waalimu wa sheria, akawauliza, “Kristo atazaliwa wapi?”
Mathayo 2:3-4 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye. Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi?
Mathayo 2:3-4 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye. Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi?
Mathayo 2:3-4 NEN (Neno)
Mfalme Herode aliposikia jambo hili aliingiwa na hofu sana pamoja na watu wote wa Yerusalemu. Herode akawaita pamoja viongozi wa makuhani na walimu wa sheria, akawauliza ni wapi ambapo Kristo angezaliwa.